“Kicheko cha ushindi: Mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF, Maulid Mtulia akiwa pamoja na Mawakili wanaosimamia kesi ya msingi kupinga kubomolewa kwa wakazi wa Mabondeni waliopo kwenye jimbo hilo. (Picha zote na Andrew Chale wa Modewjiblog)
 Zoezi la bomoabomoa kwa wakazi wa mabonde ya Kinondoni limesitishwa mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa katika mahakama kuu ya ardhi hapo  siku ya Jumatatu, 11 Januari. Hiyo ni baada ya Wakili huyo pamoja na wananchi hao wa Mabondeni kuwasilisha orodha kamili ya majina na anuani za nyumba zao.
Akisoma  uamuzi wa Mahakama kuu ya Ardhi, Mh. Panterine Kente  akisoma maelezo ya maamuzi ya shauri hilo, aliwataka Mawakili wanaotetea wkazi hao wa mabonde ya Kinondoni kuwasilisha orodha ya majina na anuani za zao na kuziwasilisha Mahakamani hapo kwa hatua zaidi huku akiwataka kufika Mahakamani hapo siku ya Jumatatu, 11 Januari.2016.
Mh. Jaji Kente ameeleza kuwa, Serikali si binadamu ila maamuzi yake yanaheshimiwa hivyo kwa upande wa shauri hilo, litaanza kusikilizwa mpaka hapo yatakapopelekwa majina yote kamili ya wakazi wanaopinga kubomolewa kwa hatua zaidi.
Hata hivyo, baada ya hatua hiyo, Wakazi hao walilipuka kwa shangwe za furaha baada ya kuelezwa kuwa zoezi hilo linasitishwa kwa muda kwa wakazi hao waliofungua kesi mpaka hapo itakapoamuliwa vingine.
Modewjiblog iliyokuwa kwenye tukio hilo tokea asubuhi, awali ilishuhudia wakzi hao wakiwa na nyuso za simanzi huku wasijue nini la kufanya baada ya awali licha ya Mahakam hiyo kueleza kuwa ingesikiliza ksi hiyo mapema majira ya saa tano asubuhi, lakini shughuli ya shauri hilo lilikuja kusomwa majira ya saa tisa kasoro.
Hali katika eneo hilo la Mahakama ikiwemo nje ilikuwa imeimalishwa ikiwemo magari ya vikosi vya ulinzi pamoja na lile la washawasha. Lakini wakazi hao waliendelea kusubiria nje ya Mahakama hiyo kwa amani.
DSC_0067
Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) mara baada ya maamuzi ya Mahakama kueleza kusimaamisha zoezi la ubomoaji huku wakitakiwa kuwasilisha majina ya watu wote wanaotakiwa kubomolewa  hadi siku ya Jumatatu.
DSC_0048
taswira ya mbali picha iliyopigwa kutoka juu gorofa ya saba katika jengo la NHC ilipo Mahakama kuu ya Ardhi.
DSC_0094
Moja ya magari ya vikosi vya ulinzi yaliyokuwa yakilinda, amani nje  ya Mahakama hiyo.