MSANII
KUTOKA TANZANIA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI CHINA
Kadhia ya
watanzania kujihusisha na madawa ya kulevya imeendelea kujitokeza hii ni baada
ya siku cache kuwepo taarifa kuwa mrembo almaarufu kwa jina la 'Winnie Mandela'
katika muziki wa kizazi kipya akiwa kunaswa na polisi China.
HUKU modo
maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, akisota jela nchini
China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga), mrembo mwingine
ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki wa Kizazi Kipya
almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, naye amenaswa na polisi nchini humo.
Tukio hilo
lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupitishwa kwa msako maalum wa
kutokomeza biashara hiyo katika viunga vya Mji wa Hong Kong, China.
Kwa mujibu
wa chanzo cha habari hii chenye maskani yake Hong Kong, Mbongo Fleva, Juma Khaleed ‘Jux
Vuitton’ na meneja wa msanii wa Bongo Fleva aitwaye Mirrow, Petit Man nao
walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika kuunganishwa kwenye
oparesheni hiyo ya ukamataji wa waingizaji wa madawa ya kulevya nchini China.
'Winnie
Mandela' wa muziki wa kizazi kipya Bongo akiwa chini ya ulinzi mkali China.
MADAI YA
KUBEBA UNGA
Ilidaiwa
kwamba Winnie alijikuta mikononi mwa askari wa China akidaiwa kubeba mzigo wa
unga tumboni hivyo kukamatwa na kutembezwa mitaani kuelekea kituo cha polisi.
APITA
VIZUIZI, AKAMATWA
Ilisemekana
kwamba Winnie ambaye ni msichana wa mjini Dar, alifanikiwa kupita vizuizi vyote
lakini kwa hali ilivyo kwa sasa nchini humo ndipo akajikuta akikamatwa na
kutembezwa mtaani kama mhalifu wa kivita.
“Unaambiwa
ilikuwa kama vita kwani polisi wa China huwa wana silaha za kutisha sana.
Unajua Winnie alikamatwa kwenye mitaa ambayo kuna Wabongo wengi hapa Hong
Kong,” kilisema chanzo chetu kutoka Hong Kong.
Ilidaiwa
kwamba askari hao walipokea agizo maalum kutoka kwenye kitengo cha kudhibititi
madawa ya kulevya nchini humo kwani kwa sasa nchi hiyo imechafuka kwa
uingizwaji wa madawa ya kulevya, jambo ambalo limeifanya serikali ya China
ifanye oparesheni kubwa ya kuhakikisha wanatokomeza wimbi hilo.
KWA WABONGO
CHINA
Chanzo chetu
kilisema kwamba kwa sasa Wabongo wanaokwenda au wanaokaa China wanaishi kama
digidigi kwani wamefikia hatua ya kutoonesha pasipoti zao na hata wengine wanadiriki kukataa uraia
wao kwa kuwa Wabongo ndiyo wanasakwa kwa wingi.
“Sasa hivi
jamaa wakisikia huyo ni Mtanzania wanamfuatilia sana kwani ndiyo wenye sifa ya
uingizaji wa dawa za kulevya nchini China,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
KAMA HUAMINI
MUULIZE JUX AU PETIT MAN
“Hicho
ndicho kilichomtokea Winnie. Nakwambia Wabongo wanazidi kukamatwa na madawa ya
kulevya. Yaani ni aibu, huwezi kuamini.
“Wabongo
wengi sana wamekamatwa Hong Kong na wengine familia zao Bongo hazijui.
“Kama
Watanzania hawaamini wawaulize Jux na Petit Man ambao walishuhudia mtiti mwanzo
mwisho.”
BALOZI WA
TANZANIA CHINA
Ili kupata
undani na idadi ya Watanzania wanaokamatwa kwa ishu za madawa ya kulevya nchini
China, chanzo cha habari hii kilimtafuta Balozi wa Tanzania China, Luteni
General Abraham Shimbo ambapo simu yake ya ofisini iliita bila kupokelewa.
Wakati Jack Patrick akisubiri kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine mwezi
ujao, ripoti zinaonesha kwamba wapo Watanzania wengi waliofungwa na wengine
kunyongwa kwa msala wa madawa ya kulevya.
0 comments:
Post a Comment