TUKIO KATIKA HALI ILIVYOKUWA
afande mkoa wa Geita kuna tukio la mauaji KTR/ IR/1186/2015, lililotokea leo tarehe 14/11/2015 baada ya ALPHONCE S/O MAWAZO, miaka 39, msukuma, mkulima mkazi wa Geita na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita pia katika uchaguzi mkuu uliopita alikuwa mgombea ubunge jimbo la Busanda, alishambuliwa kwa silaha za jadi na watu wanaosadikiwa kuwa zaidi ya kumi kati yao mmoja ametambuliwa kwa jinamoja la MABEGA, wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa CCM.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa CHADEMA walikuwa na mkutano wao wa ndani katika mtaa wa Ludete A kata ya Ludete katika mji mdogo wa Katoro na CCM pia walikuwa na mkutano na ndani katika ofisi ya CCM, mtaa wa Njiapanda kata ya Ludete, vyama vyote viwili vilikuwa vinaandaa na kuwaapisha mawakala wao kwa ajili ya uchaguzi wa diwani ambao utafanyika kesho tarehe 15/11/2015 katika kata ya Ludete.
Wakati mkutano wa chadema ukiendelea majira ya 12:35 hrs mwanachama mmoja wa CHADEMA alitoa taarifa kuwa nje ya ukumbi kuna watu wanaosadikiwa kuwa wanachama CCM wanarekodi mkutano wao. Baada ya taarifa hiyo wajumbe wote walitoka nje ya ukumbi wakakutana na kundi la hilo nje ya ukumbi. Watu hao waliwashambulia kwa silaha butu 1.
ELIZABERT D/O PASCHAL, miaka 43, msukuma,mkulima wa Katoro ameumia kisogoni 2. BAHATI S/O MICHAEL, miaka 38, mzinza, mkulima mkazi wa Katoro, amejeruhiwa kichwani. Wametibiwa kituo cha afya Katoro, wameruhusiwa na hali zaozinaendelea vizuri. Kutokana tukio hilo wajumbe wote wa CHADEMA walitawanyika.
Marehemu alitoweka katika eneo hilo katika mazingira ambayo hata wenzake wameshindwa kuyaelezea. Muda mfupi alionekana akipigwa katika umbali unaokadiliwa kuwa nusu kilometa kutoka ukumbi ulipokuwa unafanyika mkutano wao na watu kumi walioshuka kwenye gari aina ya Land Cruiser ambayo namba zake bado hazijafahamika. Baada ya tukio hilo gari hilo lilielekea barabara ya Geita mjini.
Majeruhi alifariki majira ya saa16:00 hrs wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya Geita.Upelelezi wenye kuambatana na msako mkaliunaemdelea kuwatafuta watuhumiwa.
SOURCE GOODRUCK PETER GROUP LA KAMBI RASMI YA LOWASA
0 comments:
Post a Comment