Serikali ya Uganda imetishia kuwakamata
wafuasi wa kinara wa chama cha upinzani cha “Forum For Democratic Change” (FDC)
Dkt Kiiza Besigye.
Utawala wa rais Yoweri Museveni umesema
utawakamata wale wanaojiunga katika vikundi wakati wa kuhesabu kura
kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi ujao.
Hayo yanajiri wakati wafuasi wa chama tawala
cha NRM kwa mara nyingine wamevamia mikutano ya wagombea urais wa upinzani Dkt
Kiiza Besigye na Amama Mbabazi na kutatiza hotuba zao.
Toka kuanza kwa kampeni za urais nchini
Uganda kumekuwa na ghasia baina ya wafuasi wa vyama vya siasa vinavyowania
kupata kura nyingi na wagombea wao kushinda katika uchaguzi ujao.
Unaweza kusikiliza sauti ya mwandishi wetu wa
Kampala, Kennes Bwire kuhusiana na heka heka za uchaguzi wa Uganda.
0 comments:
Post a Comment