Wanachama wa CCM katika Jimbo la Ludewa
mkoani Njombe, leo wanapiga kura za maoni ili kumpata mgombea ubunge kupitia
chama hicho atakayeziba pengo lililoachwa na Deo Filikunjombe aliyefariki
dunia Oktoba 15, mwaka huu.
|
Makada 10 wa CCM waliochukua na
kurejesha fomu wanatarajiwa kupigiwa kura na wanachama wa CCM ili kumpata
mgombea atakayepambana na wagombea wa vyama vya upinzani.
|
Makada hao ni Philip Filikunjombe
(mdogo wa Deo Filikunjombe), Edgar Lugome, Johnson Mgimba, Emmanuel Mgaya,
James Mgaya, Jackob Mpangala, Simon Ngatunga, Evaristo Mtitu, Deo Ngalawa na
Zephania Chaula.
|
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Ludewa mjini, Tafuteni Mwasonya alisema
kuwa tayari Mungu amekwishawapatia wananchi wa Ludewa mbunge na
kinachosubiriwa ni taratibu za kidunia zifanyike.
|
Alisema wananchi wanapaswa
kumuomba Mungu badala ya kusikiliza maneno yasiyo na maana, kwa kuwa
anayetakiwa ni mtu anayeifahamu vizuri Ludewa na mwenye uchu wa kuwaletea
maendeleo. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti jana,
baadhi ya wananchi walisema imani na matumaini yao ni kuona wajumbe wa
mkutano wa CCM wanamchagua mtu anayekubalika.
|
Mmoja wa wakazi hao, Bruno Mtega
alisema wanaamini kuwa mtu atayechaguliwa na wana CCM atakuwa mshindani mzuri
miongoni mwa wagombea ubunge watakaopigiwa kura.
|
John Haule anayeishi Mavanga mjini
hapa, alisema wagombea wote wana nafasi sawa, lakini yupo mmoja ambaye ni
zaidi ya wote kwa kila kitu
|
Alisema licha ya kumpoteza
Filikunjombe, wana nafasi ya kuchagua mtu ambaye atafanya vizuri zaidi miaka
mitano ijayo.
|
Home
»
»Unlabelled
» MRITHI WA FILUKUNJOMBE KUPATIKANA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment