Mfumo wa Benki ya Wananchi wa
Vijijini (Vicoba), Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro unakabiliwa na
changamoto za ukosefu wa mitaji na kusabaisha wanachama wake kuwa maskini.
Mkurugenzi
na Mwezeshaji wa Taasisi inayosimamia mfumo wa Vicoba ya Nyote, Wilaya za
Manispaa ya Moshi na Moshi Vijijini, Erasimo Njafula alisema hayo jana
kwenye mkutano uliofanyika katika Kata ya Njiapanda.
Alisema
baadhi ya wanachama siyo waaminifu kwani hushindwa kurejesha fedha
walizokopeshwa kwa ajili ya kuendeshea miradi yao, hali inayokwamisha
wanachama wengine wasipate mikopo kwa wakati.
Alisema
mfumo huo kwa Mkoa wa Kilimanjaro, ulianza mwaka 2007, hivyo changamoto
zilizopo zinasababisha wanavikundi kurudi kwenye hali ya umaskini.
Baadhi
ya wanavicoba wa Vunjo, walitaka ahadi ya fedha iliyotolewa na Rais John
Magufuli kwenye vikundi vya vikoba ambavyo vimesajiliwa, itekelezwe.
Akiwa
katika mkutano wa kampeni mwezi uliopita uliofanyika Uwanja wa Mashujaa
Manispaa ya Moshi, Rais Magufuli aliahidi kuwa iwapo atachaguliwa atahakikisha
anatoa Sh50 milioni kwa kila kata ili ziweze kusaidia wananchi kujikwamua
na umaskini.
Mwanachama
wa Kikundi cha Vicoba cha Tupendane, Eskari Ndossy aliitaka Serikali itenge
fedha kwa ajili ya kusaidia vikundi hivyo.
Hadi
sasa Manispaa ya Moshi ina vicoba 118 vilivyounganisha rasilimali zao kwa
kuchangiana, hivyo kubuni miradi ya maendeleo ikiwamo ya upishi,biashara ya
matunda, nguo, viatu vya mitumba na usafirishaji wa abiria na mizigo kwa
kutumia bodaboda na bajaji
|
0 comments:
Post a Comment