SDL
Ligi Daraja la Pili nchini (SDL) iliaanza kutimua vumbi wikiendi iliyopita katika viwanja 12 mikoani.
Ligi Daraja la Pili inashirikisha vilabu 24 ambavyo vinasaka nafasi nne za kupanda Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao wa 2016/2017.
Katika michezo iliyochezwa wikiendi, matokeo yalikuwa ni Alliance 2 -0 Madini, JKT Rwamkoma 1- 3 Bulyanhulu, Mvuvuma 0 – 0 Green Warriors, Singida United 1 -0 Transit Camp, Mirambo 1 – 0 Abajalo Tabora.
Karikaoo 1 – 0 Cosmopolitan, Mshikamano 1- 1 Changanyikeni, Villa Squad 0 – 2 Abajalo Dar es salaam, Mkamba Ranger 0 -0 The Mighty Elephant, Sabasaba 0 – 1 Mbeya Warriors, Wenda 0 – 0 African Wanderes.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea Novemba 28, kwa timu 24 kucheza katika viwanja 12 mbalimbali nchini kusaka pointi muhimu.

0 comments:

 
Top