Michezo ya awali ya kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia nchini Urusi 2018 kwa ukanda wa Afrika, zimepigwa usiku wa kuamka leo.
Tanzania wakicheza ugenini dhidi ya Algeria walikubali kichapo cha mabao7-0 na kufuta kabisa ndoto zao za kusonga mbele.
Timu ya taifa ya Kenya Harambee Star nao wakalala kwa kufungwa mabao 2-0 na Cape Verde.
Rwanda wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wakafungwa na Libya kwa mabao 3-1.
Matokeo mengine ya michezo hiyo ni
Cameroon 0-0 Niger, Congo 2-1 Ethiopia ,Nigeria 2-0 Swaziland,Ghana 2-0 Comoro.
Misri 4-0 Chad, Ivory Coast 3-0 Liberia, Tunisia 2-1 Mauritania, South Africa 1-0 Angola.
Burkina Faso 2-0 Benin, Senegal 3-0 Madagascar, Mali 2-0 Botswana
0 comments:
Post a Comment