Washington, Marekani.Watu watano waliokuwa wanashikiliwa kwenye Gereza la Guantanamo Bay kwa zaidi ya miaka 13, wameachiwa huru na wamepelekwa katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema kuwa watu hao raia wa Yemen, walikubaliwa kupata makazi kwenye taifa hilo la Ghuba ya Uajemi, baada ya Marekani kuona kwamba sio tena tishio kwa Marekani.



Sehemu ya uzio wa gereza la Guatanamo.
Kuachiliwa kwa watu hao kunalifanya gereza hilo sasa kuwa na wafungwa 107. 

Watu hao waliowasili katika Umoja wa Falme za Kiarabu Jumamosi, walitambuliwa kwa majina yao ambayo ni Ali Ahmad Muhammad al-Razihi, Khalid Abd-al-Jabbar Muhammad Uthman al-Qadasi, Adil Said al-Hajj Ubayd al-Busays, Sulayman Awad Bin Uqayl al-Nahdi na Fahmi Salem Said al-Asani. 

Hakuna yeyote miongoni mwao aliyefunguliwa mashtaka ya uhalifu, lakini wamekuwa wakishikiliwa kama wapiganaji maadui.

Kwenye gereza hilo mfungwa hufungwa kwenye kiti cha chuma na kulishwa kwa kutumia mipira inayopitishwa puani.

Wafungwa wengi wa kijeshi na kisiasa, hasa wale wanaopingana na itikati za Magharibi ndio wanakutana na adha ya gereza hili.

0 comments:

 
Top