Napenda Niwe Nakutumia Kila Habari Mara tu Ikitoka ..Bofya HAPA Ujiunge Nami SASA..
Chopa iliyombeba naibu waziri wa fedha namgombea ubunge jimbo la Iramba Magharibi,Mwigulu Nchemba na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza Anthony Diallo leo jioni waliokuwa wameambatana na mbunge wa Viti maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal ikitua katika eneo la Ngokolo Mitumbani kata ya Ngokolo mjini Shinyanga kwa ajili ya mkutano wa hadhara kumnadi mgombea urais wa CCM Dk John Pombe Magufuli,mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele na mgombea udiwani wa kata hiyo Emmanuel Mlimandago Dominic-Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akiwapungia mkono wananchi wa Shinyanga waliojitokeza leo Oktoba 12,2015 katika mkutano wa hadhara eneo la Ngokolo Mitumbani mjini Shinyanga.
Akiwa Shinyanga Mwigulu Nchemba aliwaasa wakazi wa Shinyanga kutopoteza kura zao kwa kuchagua wagombea wa upinzani bali wachague rais,wabunge na madiniwa wa CCM huku akimwelezea mgombea ubunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele kuwa ni jasiri,msikivu,mchapakazi,mwenye uzoefu wa kazi,muungwa,mwadilifu na mwenye kiu ya kuwaletea maendeleo wananchi hivyo wampe kura na kwamba ndiye mgombea pekee aliyepata mafunzo mengi ya uongozi.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akiwahutubia wakazi wa Shinyanga leo jioni ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wananchi kutunza kadi zao za kupigia kura na kujitokeza kwa wingi kuchagua wagombea wa CCM
Kushoto ni mgombea ubunge jimbo la Solwa Mheshimiwa Ahmed Salum akiteta jambo na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kwenye mkutano
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba pia aliwataka watanzania kupiga kura kwa kutumia vigezo mbalimbali ikiwemo uwezo wa uchapa kazi wa wagombea,uadilifu wao ambapo alielekeza sifa hizo kwa wagombea wa CCM akiwemo John Pombe Magufuli
Mheshimiwa Nchemba alisema kuwa mgombea urais wa Ukawa Edward Lowassa na wenzake wamehama CCM kwa sababu ya hasira ya kukosa urais kupitia CCM na kwamba CCM siyo mbaya...na kama ingekuwa mbaya wasingezunguka nchi nzima kusaka wadhamini wakati wa mchakato wa kupata wagombea wa chama hicho.
Wagombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini na Solwa Stephen Masele na Ahmed Salum (kulia) wakifuatilia kwa umakini zaidi hotuba ya mheshimiwa Mwigulu Nchemba
Mkutani unaendelea
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akimsikiliza mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele baada ya kumaliz hotuba yake
Wafuasi wa CCM wakifurahia jambo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Diallo akiwahutubia wakazi wa Shinyanga leo ambapo alisema Chadema imepoteza mwelekeo kwa kumuweka Lowassa kuwa mgombea wao huku akisisitiza kuwa Lowassa amenunua Chama hicho ndiyo maana hata sare za Chama huwa havai kwenye mikutano ya chama hicho
Tunafuatilia mkutano....
Mkutano unaendelea
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Diallo akimnadi mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele na mgombea udiwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Mlimandago Dominic
Mkutano unaendelea
Akina mama wakiwa eneo la mkutano
Tunashangilia CCM yetu na wagombea wetu....
Wananchi wakishangilia .....
Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wakazi wa Shinyanga kumchagua kwa awamu nyingine ili kuinua uchumi katika jimbo hilo.
Wananchi wakimshangilia mbunge wao
"Nipeni muda niwafanyie kazi,ndugu zangu ushabiki hautasaidia,epukeni kuchagua watu ambao hawana hata anuani...hawajulikani hata wanaishi wapi...Nimefanya mambo mengi Shinyanga....Nimejenga barabara,nimejenga hospitali ya rufaa ya mkoa,nimeleta viwanda,katika sekta ya elimu nako tumefanya makubwa,umeme pia...maji lakini wenzetu hawaoni haya"..alisema Masele.
Source: MALUNDE BLOG
0 comments:
Post a Comment