Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema, Edward Lowassa, katika Uwanja wa Mnadani, Jimbo la Busanda, Mkoani Geita leo Oktoba 13, 2015. 










Idadi ya Wapiga Kura bara ni 22,751,292, Zanzibar ni 503,193

Idadi ya Wagombea wa Ubunge
Jumla Wagombea 1,218 wa nafasi ya Ubunge waliteuliwa, Kati ya hao Wanaume ni 985 na wanawake ni 233.

Idadi ya Wagombea wa Udiwani
Jumla ya Wagombea 10,879 waliteuliwa kuwania nafasi za
Udiwani kati ya hao wanaume 10,191 na wanawake 679. 

Jumla ya Majimbo 264 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kata 3,957 za Tanzania Bara zitashiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
Jumla ya Wagombea 8 wa nafasi ya Kiti cha Rais waliteuliwa kuwa Wagombea kati ya hao mwanamke ni 1 na wanaume 7.
Jumla ya Vyama vya siasa tisa (9) tu ndivyo vimewasilisha fomu na majina ya wagombea wa Viti Maalum mpaka ilipofika siku ya mwisho, yaani tarehe 25 Septemba, 2015.
 Vyama hivyo ni CCM, CUF, UPDP, UMD, TLP, DP, NLD na ACT-Wazalendo. Vyama vingine mpaka sasa havijawasilisha orodha kama Sheria inavyosema. 

Jumla ya taarifa za wananchi 181,452 walijiandikisha zaidi ya mara moja hadi mara nane kwa mtu mmoja. 

Jumla ya taarifa 3,870 wamebainika kuwa waliandikishwa wakiwa sio raia wa Tanzania na hivyo, vitambulisho vyao vimerejeshwa na taarifa zao kufutwa kwenye kanzidata ya Daftari la Kudumu. 

Hivyo, jumla ya taarifa za Wapiga kura 1,031,769 zimefutwa kutokana na sababu tajwa hapo juu. 

Kwa maana hiyo, idadi halisi ya Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga la Kura ni 22,751,292 waliandikishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na 503,193 waliandikishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)
Idadi ya Vituo vya Kupigia Kura
Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Tume imeaandaa vituo vya kupigia kura 65,105, ambapo, Tanzania Bara ni Vituo 63, 525 na Zanzibar ni Vituo 1,580. 
Kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia Wapiga Kura 450 na wasiozidi 500.

0 comments:

 
Top