HATUA ZA KUFUATA SIKU YA KUPIGA KURA:
1. Ukifika kituoni panga mstari, isipokuwa walemavu, wazee, wajawazito na wanaonyonyesha.
2. Mkabidhi msimamizi wa kituo kadi yako ya kupigia kura ili aihakiki.
3. Msimamizi wa kituo asome jina lako kwa sauti.
4. Mawakala wote wa vyama vya siasa wasikie, wakiwa na shaka wakuhoji.
5. Pokea karatasi tatu za kupigia kura, endapo wagombea wote wanashiriki.
6. Nenda kwenye kituturi (chumba) ambako kuna faragha na utulivu.
7. Kwa kila nafasi, weka alama ya vema kwa mgombea unayemtaka.
8. Kunja na utumbukize kila karatasi kwenye sanduku husika; urais, ubunge na udiwani.
9. Chovya kidole kidogo cha mwisho cha kushoto kwenye wino maalum.
10. Ondoka kituoni. Nenda nyumbani kusubiri matokeo.
0 comments:
Post a Comment