Chief Jaji Madam Rita (kushoto) akiwa na mshindi mpya wa msimu wa wa nane wa shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search BSS, Kayumba Juma katikati alieshika mkoba wa fedha kiasi cha sh Milioni 50 za Kitanzania.
mshindi wa shindano la BSS 2015 ameshapatikana ambaye ni kijana mdogo kabisa Kayumba Juma aliweza kuteka hisia za watu katika uimbaji wake tokea kuanza kwa mashindano hayo hadi kufikia fainali.
Katika fainali hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa mpya kabisa wa King Solomon Hall uliopo Bamaga, uliweza kushuhudia washiriki 6 waliongia hatua ya fainali kuchuana vikali kuwania kitita hicho cha milioni 50. Hata hivyo mwishowe washiriki wawili Nasseb Fonabo na Kayumba Juma waliweza kuchuana na hatimae Chief Jaji, Madam Rita alimtangaza Kayumba kuwa ndiye mshindi wa kwa mwaka huu wa BSS 2015.
Pichani chini ni picha za matukio hayo baada ya Kayumba kutangazwa kuwa mshindi
Pichani ni muda mfupi kabla ya Chief Jaji Madam Rita kuanza kutangaza mshindi wa shindano hilo.
Kayumba akishangilia kwa shangwe baada ya kutangazwa kuwa ndiye mshindi wa shindano hilo
Kayumba akilia kwa uchungu baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi..
Kayumba kwa furaha aliweza kumrukia mshiriki mwenzake alieingia naye hatua ya mbili bora, Fonabo
Madam Rita akimbembeleza Kayumba
Hatimaye aliweza kunyakua mkwanja kamili wa Milioni 50 na kukabidhiwa
Wanahabari wakiendelea kuchukua matukio hiyo ilikuwa ni majira ya usiku wa saa nane na dakika 21 lakini watu walikuwa ni wengi na wako macho wakifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea bila kulala.
0 comments:
Post a Comment