Baada ya kuhitimisha kwa kishindo kanda ya kaskazini sasa ni rasmi kanda ya ziwa akianzia Tarime mkoani Mara.
Edward Lowasa anayetajwa kama mkombozi wa Tanzania ijayo, amesema ni dhamira yake kuona mtanzania akineemeka na keki ya taifa huku suala la elimu kwake akisema ndio itakuwa slaha kubwa ya kuifikisha Tanzania panapotakikana.
Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu amesema wanatarime na watanzania kwa ujumla hawanabudi kuitumia vema Oct 25 kwa kukiondosha chama cha CCM kwani kuna kila dalili ya kuchokwa na watanzania.
Mhe. Edward Ngoyai Lowassa akiwasili Tarime mkoani Mara na kupokelewa na wananchi wa Tarime kwa shangwe,vifijo na nderemo wakiimba Rais...Rais...Rais..huku wakielekea kwenye uwanja mkutano wa 77 Tarime mjini Jumamosi 10/10/2015
"Tarime tunataka maji tumaini letu ni Lowassa" Leo Jumamosi 10/10/2015
Mhe. Edward Ngoyai akiwanadi wagombea udiwani Mugumu wilaya ya Serengeti Jumamosi 10/10/2015
Mgombea jimbo la Tarime mjini Ester Matiku akiongea na Wanatarime , katika viwanja vya 77 Tarime mjini, tarehe 10/10/2015
Edward Ngoyai Lowassa akiongea na wananchi wa Tarime mjini katika viwanja vya 77 Jumamosi 10/10/2015
0 comments:
Post a Comment