PICHA--,tizama mkutano wake hapa
Mgombea udiwani katika kata ya mbagala Kuu akimwaga serera mbele ya wakazi wa Mbagala katika viwanja vya Zakiem jioni ya leo |
Mgombea Udiwani Kata ya Mbagala Kuu kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM , Yusuphu Manji amewataka vijana wasidanganywe na mabadiliko na kudai kuwa fedha zake nyingi zitatumika kwa ajili ya kuleta maendeleo.
Akizunguza katika mkutano wa Hadhara wa kuomba ridhaa ya wana mbagala kuu amesema kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa Diwani katika Kata hiyo atahakikisha anachimba visima vingi ili kutatua changamoto ya maji ambayo imekuwa sugu katika maeneo hayo kwa sasa.
Manji ambaye katika upande wa michazo ni mwenyekiti
wa timu ya Yanga ameahidi kuwa endapo atapata ridhaa kila mwaka katika Kampuni zake atawapatia vijana ajira huku akiahidi pia kuongeza Zahanati na kuboresha huduma za afya katika kata hiyo.
Aidha katika hatua nyingine mgombea huyo ameahidi kujitolea kuwakopesha wanachi hao magari zaidi ya 20 kuzoa taka katika maeneo hayo ikiwa ni jitihada za kupambana na tatizo la usafi katika kata hiyo
Pia Manji aliongeza kuwa atawawekea wananchi wake sola,ndani ya miaka miwili ataboresha miundo mbinu shuleni huku swala la mifuko ya wakina mama atasimamia fedha zinazotengwa ili waweze kukopeshwa waendeshe biashara zao.
Katika upande mwingine naye MGOMBEA Ubunge wa jimbo jipya la mbagala Mbagala jijini Dar es Salaam,Ally Mangungu amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kumchaguwa atahakikisha anajenga Chuo Cha Ufundi Stadi ili vijana waweze kujiajiri na kuweza kufikia ndoto zao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Katika mkutano wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika viwanja vya Zakhem,Mangungu amesema hapa nchini kumekuwa na wimbi la vijana ambao hawana ajira hali inayowasababisha wajiunge katika vitendo vya uvunjifu hivyo Chuo hicho akikijenga kitasaidia kupunguza wimbi la umaskini linalowakabili vijana.
Amesema Chuo hicho kitakapojengwa kitawawezesha kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji na kuwawezesha kujitegemea na kufikia malengo yao ya maisha.
“Mbali na kujenga Chuo hicho, ntahakikisha najenga aliahidi atajenga shule ili wanafunzi wanapomaliza kidato cha nne waweze kujiunga na kidato cha tano na sita:
MGOMBEA Ubunge wa jimbo jipya la Mbagala Mbagala jijini Dar es Salaam,Ally Mangungu akizngumza katika mkutano huo |
Nakuongeza kuwa jimbo hili lina shida ya vyumba vyamadarasa ntahakikisha tunapata madarasa ya kutosha”alisema Mangungu.
Akizungumzia wanawake amesema atahakikisha anafuatilia Sh. Million 10 zinazotengwa kila mwaka na Halmashauri ya Manspaa ya Ilala ili wanawake wakopeshwe waweze kuendesha biashara zao.
0 comments:
Post a Comment