Vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi - UKAWA vimeitaka Tume ya taifa ya Uchaguzi NEC Kuunda kamati ya Pamoja ya vyama vya siasa pamoja na wataalam wa Tehama kutoka katika vyama hivyo ili kuchunguza mfumo wa Computer Utakaotumika kuhesabia kura ili kujiridhisha kutokuwepo kwa Suala la wizi na Uchakachuaji wa kura wakati wa kutoa matokeo ya Urais.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm Naibu katibu mkuu wa Chama cha demokraisa na maendeleo CHADEMA John Mnyika amesema mfumo uliopo ambao ndiyo utakaotumika katika kuhesabu kura bado wanautilia mashaka na kuitaka tume hiyo kutoa ruhusa kwa wataalam wa IT kuufanyia uchunguzi.
Kauli ya Mnyika inafuatia kauli ya Mwenyekiti wa tume ya taifa ya Uchaguzi,Jaji Damian Lubuva kwamba Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa huru na haki na hakuna suala la wizi wa kura kwa sababu ya kuboreshwa kwa mfumo utakaotumika kuhesabu matokeo ya kura ikiwemo kubandikwa kwa matokeo ya urais, ubunge na udiwani katika Vituo husika.
Aidha amesema Ukawa wanapingana na kauli ya M/kiti wa Tume kuwa baada ya upigaji kura watu watawanyike ambapo Ukawa imetoa wito kwa wafuasi wake kufuatilia matokeo ya upigaji kura katika maeneo yao.
0 comments:
Post a Comment