Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, hatua yoyote ile - hata ndogo kiasi gani - ya kuwavunjia heshima mahujaji wa Iran na kutotekelezwa majukumu yanayotakiwa kuhusiana na maafa ya mahujaji waliopoteza maisha katika maafa ya Mina, itakabiliwa na radiamali kali kutoka Iran.

Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo Jumatano katika sherehe za kula kiapo na kupewa vyeo wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya maafisa wa kijeshi wa Iran na huku akielezea kusikitishwa mno na maafa ya Mina amesema: Maafa hayo yamekuwa ni msiba mkubwa kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu na kwa taifa la Iran, kutokana na maelfu ya mahujaji kufariki dunia wakiwemo mamia ya mahujaji wa Kiirani.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia ulazima wa kuundwa kamati ya kutafuta ukweli ya nchi za Kiislamu ikiwemo Iran na kuongeza kuwa: Sisi hivi sasa hatuwezi kutoa hukumu yoyote ya kabla ya wakati wake kuhusiana na maafa hayo, lakini tunaamini kuwa serikali ya Saudi Arabia haikutekeleza majukumu yake kuhusiana na mahujaji waliojeruhiwa katika maafa ya Mina.

Ayatullahil Udhma Khamenei amesisitiza kuwa, Saudi Arabia haitekelezi ipasavyao majukumu yake kuhusiana na mahujaji waliopoteza maisha yao na kubainisha kuwa: Hadi hivi sasa Iran imeonesha subira na heshima ya Kiislamu na kuheshimu udugu ndani ya ulimwengu wa Kiislamu, lakini inabidi ieleweke vyema kwamba, itakapobidi, Iran itatumia uwezo ilio nao kuonesha radiamali yake kuhusiana na watu wanaowavunjia heshima mahujaji.

Ayatullahil Udhma Khamenei ambaye pia ni Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran amesema pia kwamba, kuwa na imani kubwa, ushujaa na elimu ni mambo matatu muhimu mno kwa ajili ya kuunda utambulisho wa vikosi vya ulinzi na kusisitiza kuwa: Kama imani itakosekana kwenye kikosi cha ulinzi, moyo wa kuua watu dhaifu nao utapata nguvu kwenye kikosi hicho.

Vile vile amesema, hatua ya kushambuliwa maeneo ya umma huko Yemen ni ushahidi wa wazi wa moyo wa kuua watu dhaifu na kukosekana ushujaa katika kikosi fulani cha ulinzi na ametoa mwito kwa vijana wa Iran waliomo kwenye vikosi vya ulinzi nchini wajiimarishe kiimani, kiushujaa, kiubunifu, kiutafiti na kielimu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Lengo la kuwa imara vikosi vyote vya ulinzi vya Iran, viwe vya jeshi, au Sepah, au Basiji au vikosi vingine vyote vya ulinzi nchini, haliishii tu katika kupata ushindi mbele ya adui, bali uimara huo unapaswa uzuie pia uchokozi na uvamizi wa maadui.

Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza kwamba, taifa la Iran limethibitisha kuwa, liko macho na linaangalia mbali katika kukabiliana na uistikbari na linaheshimu pia utambulisho wake na heshima ya wanadamu wote. Ameongeza kuwa, kusimama kidete mbele ya ubeberu kuna maana ya kulinda heshima ya mwanadamu na mataifa yote duniani.

0 comments:

 
Top