Viongozi 50 kutoka bara
la Afrika wamealikwa kuhudhuria mkutano huo wa siku tatu mjini
Washington DC, ambapo Marekani imetangaza kuwa itatoa karibu dola
bilioni moja kusaida miradi mbalimbali barani humo.
Waziri mkuu wa Guinea Mohammed Said Fofana akiwasili uwanja wa ndege wa Andrews Air force Base, Agosti 2, 2014
Marekani inatarajiwa kutangaza mabilioni ya dola za msaada kwa bara la Afrika katika mkutano wake na viongozi wa bara hilo unaoanza leo Jumatatu.
Viongozi 50 kutoka bara la Afrika wamealikwa kuhudhuria mkutano huo wa siku tatu mjini Washington DC, ambapo Marekani imetangaza kuwa itatoa karibu dola bilioni moja kusaida miradi ya kibiashara, fedha zaidi kwa walinda amani na mabilioni ya dola kwa miradi ya chakula na nishati kwa bara hilo.
China, Ulaya na Japan zote zimejaribu kutoa misaada kama hiyo ili kuinua uwekezaji Afrika lakini White house inapinga kwamba mkutano huu ni hatua ya kukabiliana na ongezeko la uwekezaji wa China barani humo.
chanzo bbc.
0 comments:
Post a Comment