Majeshi ya Israeli yakijiandaa kwa mashambulizi ya ardhini dhidi ya Wapalestina

Waziri mkuu wa Isareli Benjamin Netanyahu ameonya kuwa taifa hilo halitasita kuishambulia Gaza
 hata baada ya operesheni inayoendelea ya kuharibu njia za chini kwa chini kukamilika.

Bwana Netanyahu alionya kundi la Hamas kuwa serikali yake itaiadhibu vikali kundi hilo iwapo itathubutu tena kuidhuru taifa hilo la Kiyahudi.

Matamshi hayo yanawadia huku kukiwa na hofu huenda mazungumzo ya kusitisha mapigano yanayoendelea huko Misri yakagonga mwamba.Zaidi ya wapalestina 1,655 na waisraeli 65 wamepoteza maisha yao tangu mapigano hayo yaanze yapata majuma matatu yaliyopita .


Wapalestina wakitizama mabaki ya jengo lililolipuliwa na Israeli

Kufikia sasa Wapalestina 8,900 wa,ejeruhiwa katika makabiliano hayo .
Israeli inaendeleza kampeini ya kumtafuta mwanajeshi wake mmoja aliyetekwa nyara na wapiganaji wa Hamas , Hadar Goldin, Ijumaa iliyopita.

Israel ilianza kuishambulia ukanda wa Gaza mnamo Julai tarehe 8 ikidai ilikuwa inakusudia kusitisha mashambulizi ya mara kwa mara ya mizinga na roketi kutoka ukanda wa Gaza.

Hata hivyo Israeli ilianzisha mashmbulizi ya angani majini na ardhini mara hii ikidai kuwa ilikuwa inalenga kuharibu njia za chini kwa chini za kundi la Hamas ikidai ndizo zinazotumika kuishambulia.
CHANZO BBC

0 comments:

 
Top