Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesisitiza juu ya udharura wa kutekelezwa kivitendo makubaliano ya amani yaliyotiwa saini hivi karibuni. 

Andre  Nzapayeke amesema kuwa, ana matumaini makubaliano ya amani yaliyotiwa saini na wawakilishi wa makundi yote katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yataanza kutekelezwa haraka iwezekanavyo.

 http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/6fd0dd15efcba242c535c79301995833_XL.jpg
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameashiria baadhi ya malalamiko na upinzani dhidi ya makubaliano hayo likiwemo suala la upokonyaji silaha na kubainisha kwamba, hapana shaka kuwa daima kuna watu ambao hufanya njama za kuvuruga makubaliano, lakini la msingi ni kuwa, makubaliano hayo yametiwa saini na viongozi wa makundi yote yaliyoshiriki katika mkutano wa Jamhuri ya Congo Brazzaville.

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameutaka Umoja wa Mataifa kutoa ushirikiano unaotakiwa likiwemo suala la kuhitimisha mapigano na machafuko.

Ikumbukwe kuwa, karibu wawakilishi 170 wa upande wa serikali na wapinzani walikutana tarehe 21 hadi 23 mwezi huu katika mkutano wa “Maridhiano ya Kitaifa na Mazungumzo ya Kisiasa” katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo Brazzaville na kufikia makubaliano ya kurejesha amani na utulivu katika nchi yao.

0 comments:

 
Top