Liverpool iliwalaza mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza
Manchester City mabao 3-1 kwa mikwaju ya penalti timu hizo
zilipokutoshana nguvu 2-2 katika muda wa kawaida katika mechi ya
kirafiki ya kuwania taji la mabingwa wa kimataifa (International
Champions Cup).
Kiungo cha kati wa Liverpool ,Jordan Henderson aliisawazishia timu yake kabla ya Jovetic kuirejeshea City uongozi .
Uongozi huo hata hivyo haukudumu kwa muda mrefu kwani Raheem alifanya mambo kuwa 2-2.
Waandalizi waliamua mechi hiyo ikamilishwe kwa kupiga matuta ya penalti.
Na hapo vijana wa Brendan Rodgers walitamba na kujikatia tikiti ya nusu fainali ambapo sasa watachuana na AC Milan ya Italia .
City sasa itakwaruzana na Olympiakos ya Ugiriki.
Mchuano huo unajumuisha timu 8 za kimataifa.
Source BBC
0 comments:
Post a Comment