Zaidi ya watu 200 wanahofiwa kukwama katika
maporomoko ya udongo nchini India,huku 20 wakithibitishwa kufariki dunia
katika kijiji cha kijiji cha Malin karibu na mji wa Pune lilikotokea janga hilo.
Kazi ya uokoaji inaendelea katika eneo hilo huku hali ya hewa mbaya ikidaiwa kuchelewesha harakati hizo.
Mwandishi wa BBC Devidas Desh pande aliyepo katika eneo la tukio anasema jingo pekee linaloonekana kunusurika na janga hilo ni ya shule pekee, huku maeneo mengine yakiwa tambarale kabisa.
Narendra Modi ni waziri mkuu wa India na hapa anaelezea hatua wanazozichukua.
Maporomoko ya ardhi ni jambo la kawaida kutokea nchini India hasa kipindi cha mvua zitokanazo na pepo za Monsoon ambazo hunyesha kuanzia mwezi june hadi septemba kila mwaka.
Chanzo BBC
0 comments:
Post a Comment