Kamanda wa M23 ajisalimisha Uganda
Maafisa wa Serikali ya Uganda wanasema kuwa kamanda
wa kijeshi wa wapiganaji walioshindwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,
DRC, M23, amejisalimisha kwa utawala wa Uganda.
Ripoti
kutoka Uganda zinasema kuwa mamia ya wapiganaji wamejisalimisha pamoja na
kiongozi wao, Sultani Makenga.
Wapiganaji
hao wamejisalimisha katika eneo la hifadhi ya Wanyama ya Pori ya Mgahinga,
kwenye mpaka wa Uganda na DRC.
Mnamo
Jumanne M23 walisema kuwa wamesitisha maasi yao ya miezi 20 Mashariki mwa
Congo, baada ya kutimuliwa katika ngome zao Mashariki mwa Congo na wanajeshi wa
Serikali wakishirikiana na askari wa kudumisha amani wa Umoja wa Mataifa.
Hata
hivyo serikali za Uganda na DRC hazijaweza kuthibitsha madai haya.
Mapema
wiki hii, M23 ilisema kuwa inamaliza uasi wake wa miezi kumi na tisa masaa
chache baada ya majeshi ya serikali kudai ushindi dhidi ya waasi hao.
Ripoti
zinasema kuwa Sultani Makenga na waasi wengine 1,700, wamesalimisha silaha zao
na wanazuiliwa na jeshi la Uganda katika kambi ya jeshi ya Mgahinga, karibu na
mpaka na DRC.
Hata
hivyo Uganda imekuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani kati ya waasi na serikali
ya DRC , ingawa hakuna mkataba wa amani umefikiwa.
SOURCE BBC
0 comments:
Post a Comment