Kufuatia
kifo cha msanii nguli wa vichekesho nchini, Mzee Amri Athumani aliyeaga
dunia jana usiku majira ya saa 2:00 usiku katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akitibiwa, mtoto wa
marehemu ametoa ratiba ya kuaga na mazishi ya nguli huyo.
Mwili
wa Marehemu Mzee Majuto utaswaliwa na kuagwa katika Msikiti ulipo ndani
ya Hospitali ya Muhimbili wakati wa Swalat Dhuhr (Swala ya Mchana) leo
Agosti 9, 2018 na baadaye utapelekwa katika Viwanja vya Karimjee
vilivyopo Posta jijini humo kwa ajili ya waombolezaji wengine na
mashabiki zake kupata fursa ya kumuaga.
Baada
ya Swalat L’laasir (Swala ya Alasiri), majira ya saa 9 mchana mwili wa
marehemu Mzee Majuto utasafirishwa kwenda nyumbani kwake Mkoani Tanga
ambako maziko yatafanyika kesho Ijumaa baada ya Swalat Dhuhr ( Swala ya
Mchana) Tanga Mjini.
TAFADHARI TOA MAONI YAKO HAPA
0 comments:
Post a Comment