Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akifungua hafla ya uzinduzi wa bodi ya maji bonde la kati. Hafla hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aqua Resort Vitae mjini hapa. Kulia ni Mwenyekiti  mpya wa bodi ya maji bonde la kati, Eng.Samson Babala na kushoto ni Naibu Katibu TAMISEMI, Eng.Emmanuel Kalobelo.
IMG_1979
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Eng.Emmanuel Kalobelo, akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya maji bonde la kati uliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aqua Resort Vitae mjini hapa. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti mpya wa bodi ya maji bonde la kati, Eng.Samson Babala, wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone na kushoto ni Mwenyekiti mstaafu bodi ya maji bonde la kati, Eng.Mwanaasha Ally.
IMG_1965
Mwenyekiti mstaafu wa bodi ya maji bonde la kati, Eng.Mwanaasha Ally, akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya maji bonde la kati iliyofanyika mjini hapa jana.Kushoto walioketi  ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Eng.Emmanuel Kalobelo, katikati ni Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti mpya bodi ya maji bonde la kati, Eng.Samson Babala.
IMG_1961
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya maji bonde la kati waliohudhuria hafla ya uzinduzi bodi hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aqua resort vitae mjini hapa.(Picha na .Nathaniel Limu).
IMG_1969
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU wa mkoa wa Singida, ameuhimiza uongozi mya wa bodi ya maji bonde la kati kufanya maandalizi ya kina yatakayowezesha kupata mbinu na njia za kisasa za kusimamia na kugawa maji,ili kuepusha migogoro ya maji.
Dk.Kone ametoa rai hiyo wakati akizindua bodi ya nne ya maji bonde la kati.Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Aqua Vitae Hoteli mjini hapa.
Alisema Tanzania inalenga kwenda kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,mojawapo ya vichocheo vikubwa katika kufikia malengo hayo,ni mapinduzi ya kilimo na viwanda ambavyo yatahitaji maji mengi  na ya kutosha.
Dk.Kone alisema pamoja na kilimo na viwanda kuhitaji maji ya kutosha,pia ongezeko la watu na shughuli zao mbalimbali zikiwemo za kiuchumi,zinazitaji kiwango kikubwa cha maji.
“Kutokana na uhitaji huo mkubwa wa maji,uwezekano wa kutokea kwa migogoro itakayotokana na uhitaji wa maji,ni mkubwa.Nina taarifa kuwa tayari migogoro hii imeanza kuongezeka hasa katika maeneo ya mikoa ya Manyara na Arusha.Bodi hii ni lazima isimamie kikamilifu masuala haya kwa ukamilifu na ufanisi mkubwa”,alisema.
Katika hatua nyingine,mkuu huyo wa mkoa alisema maamuzi mengi duniani ambayo ni pamoja na yanayohusu maji,yanafanywa na wanasiasa au na viongozi ambao ni wanasiasa.
“Kwa hiyo katika utendaji kazi wenu,hamna budi kushirikiana na wanasiasa na viongozi wengine wa serikali katika ngazi za kitaifa,mikoa,wilaya,kata na vijiji,ili kutatua changamoto za maji kwa pamoja”,alisema.
Aidha,Dk.Kone ametoa rai kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, katika bajeti ya maji watoe kipaumbele katika utunzaji na usimamizi wa rasilimali za maji, ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu za maji kwa wingi.
“Bila takwimu za muda mrefu na sahihi,usimamizi wa rasilimali za maji utakuwa ni mgumu sana na unakuwa sio wa kisayansi”,alifafanua Dk.Kone.
Awali Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Eng.Emmanuel Kalobelo, alisema majukumu ya msingi ya bodi ya maji za mabonde,ni kusimamia,kupanga na kuendeleza rasilimali za maji zilizoko katika mabonde.
“Bodi hizi zikifanya kazi zake vizuri,Watanzania tutakuwa na uhakika wa uatikanaji endelevu wa maji,kwani bodi hizi ni lazima zitayarishe miango ya usimamizi wa rasilimali za maji katika mabonde.
Akifafannua zaidi, Eng.Kalobela,alisema bodi za maji za mabonde zinaaswa kushirikiana na wadau wengine kutatua migogoro ya utunzaji wa maji inayojitokeza katika maeneo yao.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu huyo, Tanzania ina mabonde tisa, ambayo ni bonde la Pangani, Ruvuma, waMi ya kusini, Rufiji, Wawi/Ruvu, Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa, Ziwa Rukwa, Ziwa Tanganyika na bonde la kati.