BAADA ya Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kufanya ziara ya kushitukiza katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kubaini upotevu wa Makontena 329, mapya yaibuka kwa Makampuni 43 kuhusika kukwepa kodi ya Sh.Bilioni 12.6 katika Bandari Kavu inayomilikiwa na Said Salim Bakhressa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa kampuni hizo 43 zilipitishiwa Kontena katika Bandari Kavu ya Said Salim Bakhressa na kutaka ndani ya siku sita kuanzia leo kampuni zote ziwe zimeshalipia kodi kutokana na idadi ya kontena.

Dk. Mpango amesema katika kampuni ambazo zilizokwepa kodi ambazo zilipitisha Kontena 329 wameshalipa zaidi ya Sh. Bilioni Tano(5) ambapo wanatakiwa kulipa kodi iliyobaki kuweza kumaliza kodi ya Sh.Bilioni 12.6 kwa kipindi alichoweka Rais Dk .John Pombe Magufuli. 
 
Kampuni zilizokwepa Kodi ya mapato kwa makontena 329 ni Lotai Steel Tanzania LTD yenye makontena 100,Tuff Tyres Centre Company kontena 58 Binslum Tyres Company LTD, Kontena 33, Tifo Global Mart (Tanzania) Company Limited Kontena 30,IPS Roofing Campany Ltd Kontena 20,Rashywheel Tyre Center Com.Ltd Kontena 12, Kiungani Trading Company Ltd 10 Homing International Limited Kontena 9, Red East Building Kontena Saba,Tybat Trading Co Ltd, Kontena Tano,Zing Ent Ltd,Kotena Nne,Juma Kassem Abdul, Kontena Tatu, Salum Continental Co.Kontena Mbili, Zuleha Abbas Ali Kotena Mbili na Snow Leopard Building Kontena mbili na waliobaki walikuwa na kontena moja moja.

Hata hivyo TRA imewasimamisha kazi watu 35 wakiwemo 27 waliokamatwa katika geti namba tano ambao hadi sasa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano na uchunguzi .

Aidha amewataka wafanyakazi kuwasilisha mali zao ili kuweza kuangalia uwezo wake katika utumishi kama zinaendana na umiliki huo.

0 comments:

 
Top