Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika nchini Comoro  amekutana na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Africa, Mheshimiwa Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma kuzungumzia hail ya siasa nchini Comoro. Katika Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliwasilisha taarifa ya ziara maalum aliyoifanya Comoro tarehe 1 Desemba, 2015.

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya, Mheshimiwa Mohammed Al-Dairi aliyemtembelea na kufanya nae mazungumzo jijini Johannesburg pembezoni mwa Mkutano wa China na Afrika.

0 comments:

 
Top