WAKATI Rais John Magufuli akiwa kwenye zoezi la kutumbua majipu kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), mshtuko mkubwa umetokea kufuatia kigogo mwenye wadhifa wa Artsan One (TPA) jijini Dar, Elia Eliampenda Kimaro (51) kufariki dunia ghafla kwa shinikizo la damu (presha) akiwa nyumbani kwake, Mikwambe, Kigamboni, Dar.
Kimaro
alifariki dunia Novemba 30, mwaka huu kwa uthibitisho wa daktari wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako marehemu alikimbizwa kwa ajili
ya matibabu.
Kifo
cha Kimaro kimetokea wakati kukiwa na sintofahamu kubwa miongoni mwa
wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuhusiana na utolewaji wa makontena 349
kinyemela na kuisababishia serikali kukosa mapato ya kiasi cha shilingi
bilioni 80.
Taarifa
kutoka ndani ya familia, marehemu alisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda
mrefu. Lakini ghafla alfajiri ya Novemba 30, hali yake ilibadilika na
hivyo kukimbizwa Muhimbili ambako daktari alisema alishafariki dunia.
Mwandishi aliweza kufika msibani ambapo aliwashuhudia wafanyakazi wengi wa bandarini na TRA bandarini wakiwa hapo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Baadhi
ya wafanyakazi hao, walisikika wakidai, marehemu alikuwa miongoni mwa
vigogo waliokuwa wakichunguzwa kwa utolewaji wa makontena 349 siku
chache zilizopita.
“Pia
nasikia baada ya waziri mkuu (Kassim Majaliwa) kutoa mwongozo siku zile
bandarini, watu wa usalama wa taifa walishamfuata hapa kwake mara
kadhaa na kumhoji.
"Lakini pia, kuna madai kwamba, miamala yake ya kibenki nayo ilifuatiliwa na jamaa hao ambapo walikuta pesa nyingi,” alisikika akisema mmoja wa wafanyakazi hao ambaye alipogundua kuna waandishi wa habar alifunga kinywa.
Nao
baadhi ya waendesha bodaboda wa eneo hilo, walionekana kushangazwa sana
kufuatia taarifa za kifo cha kigogo huyo, wakidai siku moja kabla,
walionana naye akiwa mzima wa afya.
Hata
hivyo, walisema mara baada ya taarifa za kifo, walishangaa kuona magari
yake ya kifahari yakiondolewa kutoka nyumbani kwake hapo:
“Labda
waliyapeleka mahali ili kupata nafasi ya kuweka maturubai ya msiba. Si
unajua majumba haya ya ghorofa, yana nafasi zaidi ya kwenda juu kuliko
upana,” alisema mmoja wa bodaboda hao.
Mwendesha bodaboda mmoja alisema: “Mzee
wa bandari alikuwa mtu poa sana. Hata madereva wa daladala zake
wameumia. Unajua jamaa alikuwa na mkwanja wa maana. Hii nyumba ya hapa
‘cha mtoto’, ana nyumba nyingine Yombo (Dar), magari ndiyo usiseme.
Yaani tumempoteza mtu muhimu sana.”
Marehemu Kimaro alizikwa Desemba 2, mwaka huu kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar. Ameacha mke na watoto wanne.
Credit: Risasi Jumamosi/Gpl
Credit: Risasi Jumamosi/Gpl
0 comments:
Post a Comment