TRIPLE A FM 88.5
HABARI KWA UFUPI
                    JUMAMOSI DESEMBA 05  SAA 11:ASUBUHI

Serikali ya Ujerumani imeeleza kufurahishwa na kasi ya kupambana na rushwa na ufisadi ya Rais John Magufuli na kuahidi kumpa ushirikiano katika masuala ya maendeleo.
Ujerumani inakuwa nchi ya kwanza ya kigeni kuvutiwa na kasi ya Rais Magufuli ambaye ameonekana kuelekeza nguvu si tu kupambana na maovu hayo tangu aapishwe Novemba 5, bali pia kuchochea maendeleo ya watu wenye kipato cha chini.
Akitoa pongezi hizo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani, Georg Schmidt  amesema Ujerumani inasubiri kuona vipaumbele vya maendeleo vitakavyoainishwa na serikali ya Rais Magufuli ili iweze kuisaidia utekelezaji.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yake ya siku tano hapa nchini, Schmidt amesema katika kipindi cha mwezi mmoja Dokta Magufuli ameweza kushughulikia masuala muhimu ya kijamii ikiwamo kuboresha huduma za afya na kuwa shughulikia wakwepa kodi.
================================================
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana Felix Ntibenda amemuagiza mkurugenzi wa mamaka ya maji Bi Ruth Koya kuhakikisha huduma ya maji inapatikana wakati wote kwenye masoko ili kuimalisha usafi na kuzuia magonjwa ya milipuko kikiwemo kipindupindu.
Ntbenda ametoa kauli hiyo wakati akizindua zoezi la usafi katika wiaya zote za mkoa wa Arusha zoezi litakalodumu mpaka desemba 9 mwaka huu ikiwa ni agizo la Raisi John Pombe Magufuri la kuimalisha usafi ili kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa kipindipindu.
Aidha Ntibenda amewaagiza watendaji wa soko la kilombero kuhakikisha wanakarabati miundombinu ya maji taka ikiwemo mifereji ili kuruhusu maji taka kutiririka vyema.


 
                                               NA
Serikali ya Iraq imeiamuru Uturuki iondoe wanajeshi wake katika eneo la mpakani karibu na mji wa Mosul ambalo linadhibitiwa na wapiganaji wa Islamic State.
Afisi ya Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi imetaja hatua ya Uturuki kuingiza majeshi maeneo ya Uturuki kuwa kuingilia uhuru na mipaka ya taifa hilo.
Mamia ya wanajeshi wa Uturuki, wakiwa na vifaru, walivuka mpaka na kuingia eneo hilo kwa lengo la kuwapa mafunzo wapiganaji wa Kikurdi nchini Iraq ambao wamekuwa wakipambana na wapiganaji wa Islamic State.
Ripoti zinasema wanajeshi 150 walikuwa wametumwa katika mji wa Bashiqa.
========================================
NA HUO NDIO MWISHO WA HABARI KWA UFUPI KUTOKA TRIPLE A FM; KWA TAARIFA KAMILI YA HABARI JIUNGE NASI SAA 3:00 USIKU….MIMI NI ……………………………

MSOMAJI………………………….MAONI…………………….
MHARIRI MKUU……………… .MAONI…………………
MHARIRI………………………….MAONI…………………..




0 comments:

 
Top