1
Viongozi wa benchi la ufundi la Azam Academy wakishiriki shughuli za usafi kwenye Zahanati ya Chamazi

Kikosi cha Azam FC leo kimetekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Mgufuli alilolitoa majuma machache kabla ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanganyika kwamba, siku ya kuadhimisha Uhuru wa Tanganyika December 9 wananchi wote wafanye usafi kwenye maeneo yanayowazguka ili kuzuia magonjwa mbalimbali yasababishwayo na uchafu.
Katika kutekeleza agizo hilo la Rais Magufuli, kikosi cha Azam FC kwa kushirikiana na wananchi leo kimefanya usafi kwenye Zahanati ya Chamazi iliyopo eneo la Chamazi-Mbande, Manispaa ya Temeke kwa kusafisha mazingira yanayoizunguka zahanati hiyo.

7
Wachezaji wakimwaga taka baada ya kusafisha mazingira yanayozunguka eneo la Zahanati ya Chamazi

Asilimia kubwa ya wachezaji, makocha na viongozi wengine walikuwa wanatoka katika kikosi B kutokana na kikosi cha kwanza kuwa kwenye maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba SC unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi December 12.
Mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Bi Eduiga Mroso ameushukuru uongozi wa Azam FC pamoja na wachezaji wote walioshiriki kwenye usafi wa maeneo yanayoizunguka zahanati hiyo na kuiomba timu hiyo kuendeleza ushirikiano na ujarani mwema uliopo kati yao.

6
Bi. Eduiga Mroso, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Chamazi

“Tunaishukuru timu ya Azam FC kuamua kuja kwetu kushirikiana na sisi kuunga mkono kauli ya Rais wetu Magufuli ya kuadhimisha siku ya Uhuru kwa kufanya usafi kwenye maeneo yanayotuzunguka. Lakini ushirikiano wetu usiishie hapa bali uende mbali zaidi kwasababu sisi pia ni majirani na tunawashukuru sana Azam kwa hilo kwasababu wengeweza kwenda sehemu nyingine lakini waliamua kuja kwetu”, amsesema Bi Mroso.
Kwa upande wa mtendaji mkuu wa kikosi hicho Saad Kawemba amesema wameamua kufanya usafi kwenye zahanati hiyo ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano wao na jamii hasa sehemu zenye uhitaji kama zahanati, shule na sehemu nyingine nyingi.

5
Saad Kawemba, Mtendaji mkuu wa Azam FC

Pia akaongeza kuwa, zahanati hiyo ipo eneo la jirani na wao hivyo hata ikitokea mchezaji au mtu yeyote amepatwa na maradhi atapelekwa kwenye zahanati hiyo kwa ajili ya matibabu na hicho ndio kitu kilichowasukuma kushirikiana na wakazi wa eneo la Chamazi kufanya usafi kwenye zahanati hiyo.
“Sisi kama Azam tumeamua kuja kushiriki shughuli ya usafi hapa kwasababu kwanza tunataka kudumisha ushirikiano wetu na jamii inayotuzunguka lakini pia kutekeleza agizo la Rais alilolitoa juu ya maadhimisho ya siku ya leo kwamba itakuwa ni siku ya kufanya usafi na si sherehe kubwa ya kitaifa”, amesema Kawemba wakati wa zoezi la usafi kwenye zahanati ya Chamazi.
4
“Lakini hawa ni majirani zetu, ikitokea mchezaji au kiongozi wa Azam FC akapatwa na maradhi ataletwa hapa, kwahiyo tukaona ni vyema tuje kushirikiana na majirani zetu kufanya usafi kwenye eneo la hii zahanati.

3
Wachezaji wa Azam wakisafisha mfereji (mtaro) pembeni ya zahanati ya Chamazi

Mh. Dr. Magufuli alipiga marufuku kufanyika sherehe kubwa za maadhidimisho ya siku ya Uhuru ambazo zimekuwa zikigharimu pesa nyingi na badala yake akaagiza pesa hizo zifanye kazi nyingine za maendeleo ya jamii na siku hiyo wananchi wote wafanye usafi kwenye maeneo yanayowanunguka.

2
Viongozi wa kikosi cha Azam wakishiriki zoezi la usafi lililofanyika kwenye zahanati ya Chamazi
chanzo DAUDA


0 comments:

 
Top