MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), imesema mchango wa masoko ya mitaji nchini umeongezeka kutoka asilimia 17 mwaka 2005 hadi asilimia 54 mwaka huu.
Hayo yalibainishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nasanda Massama, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kampuni ya Soko la Bidhaa (TMX), iliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete Dar es Salaam, hivi karibuni.
Alisema kwa upande wa kampuni za ndani masoko hayo ya mitaji mchango wake umeongezeka kutoka asilimia sita, mwaka 2005 hadi asilimia 24, mwaka huu.
“Hali hii inatokana na ukweli kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la kampuni zilizoorodheshwa katika masoko ya mitaji. Kwa sasa kuna kampuni 25 kutoka kampuni sita zilizoorodheshwa wakati wa kuanzishwa kwa masoko haya,” alisisitiza Massanda.
Kwa upande wake, Rais Kikwete alipongeza jitihada zinazoendelea kufanyika nchini kwa ajili ya kuboresha masoko ya mitaji, hisa na bidhaa, hali ambayo alisisitiza itasaidia kukuza uchumi wa Tanzania na kutimiza lengo la kuwa moja ya nchi zenye uchumi wa kati.
Hata hivyo, alisema pamoja na kwamba Serikali inajitahidi kukuza uchumi huo wa nchi kupitia kilimo, kutokana na Tanzania kuwa na idadi kubwa ya wakulima, bado kuna haja ya kushirikisha hadi sekta binafsi kwa ajili ya kutafuta jawabu la uhaba wa maghala ya kuhifadhia chakula.
“Nafurahi kuona namaliza muda wangu kama kiongozi wa Tanzania, lakini jitihada nilizofanya zikianza kuonekana. Sasa mageuzi ya kilimo ndio yanaanza kupitia soko la bidhaa TMX, kilimo chetu kitaimarika, lakini bila kupata jawabu la maghala ya kuhifadhia mazao, ukuaji wa kilimo utakua mgumu,” alisisitiza Rais Kikwete.
Aidha alisema sera ya kilimo kwanza inafanya vizuri, ingawa bado suala la stakabadhi ghalani limekuwa likipigwa vita, kwani wakulima wengi wamekuwa wakizalisha mazao mengi kiasi cha mengine kukosa maghala ya kuhifadhia.
“Uwezo wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ni tani 150,000 tu, lakini mazao yamekuwa mengi sana na wakulima wanafikiri kuwa NFRA ndio mnunuzi pekee wa mazao yao. Natumaini kupitia soko la bidhaa TMX, soko la mazao haya litaimarika
CHANZO HABARI LEO

0 comments:

 
Top