Dar es Salaam. Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(Suma JKT) limewataja baadhi ya wafanyakazi wa serikali wakiwamo wakuu wa mikoa,wilaya na wabunge kuwa miongoni mwa wadaiwa wanaokwamisha mradi wa matrekta kwa ajili ya Kilimo Kwanza.
Wengine wanaodaiwa kuwa kikwazo kufanikisha Kilimo Kwanza ni Taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, vikosi vya Jeshi la Kujenga Taifa na wateja waliokopa matrekta hayo kupitia mawakala.
Mkuu wa JKT,Meja Jenerali Raphael Muhunga aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya mradi wa matrekta kwa ajili ya utekelezaji wa sera ya Kilimo Kwanza.
Jenerali Muhunga alisema hadi sasa fedha wanazodai ni kiasi cha Sh41.3 bilioni
Alisema walipokea matrekta na zana yenye thamani ya Sh72.2 milioni ambapo hadi kufikia Septemba 15 mwaka huu wameuza mali zenye thamani ya Sh66 bilioni.
Hata hivyo alisema jumla ya fedha zilizolipwa kutokana na mauzo hayo ni asilimia 48.5 tu.
Mradi huo unatokana na mkopo wenye masharti kwa serikali ya Tanzania kutoka serikali ya India wenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 40 ukilenga wakulima maskini wanaotumia kilimo kisicho na tija cha jembe la mkono.
Meja Jenerali Muhunga alisema sababu kubwa ya kusuasua kwa ukusanyaji wa fedha hizo ni mradi kuwa mbali na wateja na ukosefu wa maofisa mikopo.
Mkurugenzi wa Suma JKT,Luteni Kanali Andrew Mkinga alisema mradi umefanikiwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara.
Source mwananchi comm
0 comments:
Post a Comment