Hapa ni katika viwanja vya Kanisa la Anglikana kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga ambako leo jioni mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele ameendelea na kampeni zake kuomba kura kwa wananchi ili wampatie kura ili aongoze jimbo hilo kwa kipindi cha pili.Mheshimiwa Masele alikuwa ameambatana na MNEC Gasper Kileo na mgombea ubunge jimbo la Solwa mheshimiwa Ahmed Salum wakitumia usafiri wa Chopa kutoka eneo moja na mkutano hadi jingine.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio..ametusogezea picha 22 .Mwanzo hadi mwisho wa Mkutano...Tazama hapa chini
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri eneo la mkutano
Diwani wa viti maalum Zuhura Waziri akimwombea kura mgombea urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjinin Stephen Masele na mgombea udiwani kata ya Ndala ndugu Abel Kaholwe katika viwanja vya Kanisa la Anglikana kata ya Ndala mjini Shinyanga
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UWT wilaya ya Shinyanga bi Mariam Rumatira akimwaga sera za CCM
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Sheilla Mshandete akinadi sera za CCM kwa wananchi wa Ndala leo jioni
Makada mbalimbali wa CCM wakiwa meza kuu kabla ya mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Stephen Maselea hajawasili eneo la mkutano akiwa na msafara wake wakisafiri kwa Chopa
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Sheilla Mshandete akimwombea kura mgombea udiwani kata ya Ndala Abel Kaholwe
Vijana na akina mama wakipiga Push Up Kumuunga mkono Dkt John Pombe Magufuli
Mkutano unaendelea
Waandishi wa habari Marco Maduhu na Suleimani Abei wakiwa eneo la mkutano
Kijana akiwa ameshikilia bango la Magufuli na redio yake mgongoni/kiunoni
Kulia ni Zuberi Bundala ambaye ni mjumbe wa baraza kuu la Vijana wa CCM taifa akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Ndala ndugu Abel Kaholwe
Wananchi wakiwa eneo la mkutano
Wakazi wa Ndala wakiwa eneo la mkutano
Mgombea udiwani kata ya Ndala kupitia CCM Abel Kaholwe akiwaomba kura wakazi wa Ndala ambapo pamoja na mambo mengine alitaja vipaumbele vyake kuwa ni pamoja na kuondoa kero za wananchi ikiwemo barabara mbovu,kodi za majengo,huduma za afya,maeneo kutopimwa na maji
Chopa iliyombemba mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele ikitua katika eneo la mkutano majira ya saa 12 na dakika tano jioni
MNEC Gasper Kileo akiomba kura kwa wananchi ili wawapigie kura wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao huku akisema sababu za kuchelewa kufika eneo la mkutano Ndala ni kutokana na kufanya mikutano 12 siku ya leo
MNEC Gasper Kileo akiwa na mgombea wa jimbo la Solwa Ahmed Salum jukwaani
Mkutano unaendelea
MNEC Gasper Kileo akimnadi mgombea udiwani kata ya Ndala Abel Kaholwe
Wananchi wakiwa eneo la mkutano
Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele akiwahutubia wakazi wa Ndala ambapo pamoja na mambo mengine aliwashukuru baadhi ya makada wa Chadema akiwemo kaimu katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga George Kitalama na diwani wa viti maalum kata ya Ndala Zainabu Kheri kwa kumuunga mkono na kuwaomba makada wengine wa Chadema kuendelea kumsaidia kuwashawishi wanachadema wengine wamuunge mkono mgombea huyu wa CCM kwani vile anakubalika katika jamii
Mheshimiwa Masele na msafara wake wakiondoka eneo la mkutano
0 comments:
Post a Comment