Mgombea Urais wa CCM, Dkt JOHN MAGUFULI azibomoa Ngome za CHADEMA kanda ya Kaskazini

Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mikono wananchi alipokuwa akiondoka uwanjani baada ya mkutano wa kampeni kumalizika mjini Karatu, mkoani Arusha.

Akihutubia katika kutano huo, Dk Magufuli aliwaambia wananchi wa Karatu kuwa mmoj wa viongozi wa upinzani anaowapenda kwa dhati ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa kwani ana misimamo thabiti na ana mapenzi makubwa na nchi yetu.
 

 Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Karatu, Arusha.
Wananchi wakishangilia kwa kunyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kumpigia kura za ndiyo mgombea urais wa Tbanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli mjini Karatu.

LOWASA AFUNIKA MONDULI JANA

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi, Monduli Mjini leo Oktoba 5, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli kwa tiketi ya CHADEMA, Julius Kalanga, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi,
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa, wakishiriki tendo la kimila ya Jamii ya Watu wa Kimasaai lililoongozwa na Malaigwanani.
Wananchi wa Monduli wakimpokea kwa shangwe, mpendwa wao ambaye ni Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Polisi, Monduli Mjini, leo Oktoba 5, 2015. Picha na Othman Michuzi, Monduli.

0 comments:

 
Top