Waokoaji
katika bahari ya Mediterranean wamesema kuwa hawatarajii kupata
manusura zaidi kutoka mashua iliyozama ikiwa imewabeba takriban
wahamiaji 600 katika pwani ya Libya.
Awali maafisa walihofia kuwa
huenda mamia ya wahamiaji hao walizama lakini shirika la umoja wa
mataifa kuhusu wakimbizi UNHCR limesema kuwa watu 400 waliokolewa.Jeshi la wanamaji la Italia limesema kuwa miili 25 imeokolewa hadi kufikia sasa lakini idadi ya watu wasiojulikana waliko bado haijabainika.
Zaidi ya wahamiaji 2,000 wanasemekani kufariki dunia mwaka 2015 wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kuingia Ulaya.
Kisa cha Jumatano kimetokea wakati mashua ya uvuvi iliobeba abiria kupita kiasi kukumbwa na hali mabya ya hewa takriban kilomita 25 kutoka pwani ya Libya.
Mbiu ya mgambo ilisikika mjini Sicily na boti ya kwanza kuwasili ilikuwa ilr ya wanamaji kutoka Ireland,LE Niamh.
Lakini boti hilo lilipowasili wahamiaji hao walielekea katika upande mmoja na kulifanya kuzama
Chanzo: BBC
0 comments:
Post a Comment