KAMBI YA JESHI YASHAMBULIWA KINSHASA DRC
Kumetokea ufyatulianaji mkali wa risasi katika kambi ya kijeshi katika
mji mkuu wa Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Taarifa zinasema kuwa
raia wameondolewa katika eneo hilo na haijafahamika makabiliano hayo
yaliyotokea katika kambi ya wanajeshi wa kumlinda rais yametokana na nini.
Wadadisi wa mambo
wanahisi kwamba kisa hiki huenda kikazusha utata tena kati ya Congo Kinshasa na Congo Brazzaville kwa vile shambulio
lilitokea karibu na mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Taarifa kutoka kwa
serikali zinasema kuwa wavamizi walijaribu kupenyeza katika kambi ya kijeshi
ya Camp Tshatshi na makabiliano yalizuka kwa zaidi ya
dakika 30 hivi.
Jamhuri hiyo ya
Kidemokrasia ya Congo imesakamwa na vita kwa kipindi kirefu sasa na hata rais
aliyepo madarakani kwa sasa Joseph Kabila
alichukua mamlaka baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila mwaka wa , 2001.
Majeshi yazima
shambulizi Kinshasa DRC
Duru zinasema kuwa
wavamizi takriban 20 walijaribu kuingia ndani ya kambi hiyo lakini shambulizi
likazimwa .
Raiya wamehamishwa
kutoka maeneo yaliyoko karibu na uwanja wa ndege ulifungwa wakati wa shambulizi
hilo.
Serikali bado haijamtaja
aliyehusika na shambulio hilo.
Hii sio mara ya kwanza kwa Camp Tshatshi kushambuliwa
mwaka uliyopita kami hiyo ilishambuliwa tena na wakati huo wafuasi wa dini ya
ya kikristo ya dhehebu linaloongozwa na Paul Joseph Mukungubila.
0 comments:
Post a Comment