Waafrika wanaoshtakiwa ICC
Waafrika 24 hivi sasa
wanakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ilioko The
Hague nchini Uholanzi. Hukumu moja tayari imetolewa lakini wengi wa washtakiwa
bado hawakufikishwa mahakamani kwenyewe.
Laurent Gbagbo : Rais wa zamani wa Ivory Coast yuko mahabusu
mjini The Hague tokea mwezi wa Novemba mwaka 2011.Hata hivyo mahakama imesema
hadi sasa hakuna ushahidi wa kutosha dhidi yake kuyakinisha kuhusika na uhalifu
dhidi ya ubinaadamu wakati wa machafuko yaliozuka baada ya uchaguzi wa mwaka
2010 nchini Ivory Coast.Mashtaka didi yake yanamtuhumu kwa kuhusika na mauaji
ya takriban watu 166,ubakaji,dhuluma na ukandamizaji wa wapinzani wake wa
kisiasa.
Mashtaka kama hayo
yanamkabili mke wa rais Simone Gbagbo na waziri wa zamani wa vijana Charles Ble
Goude.Wote wawili wako kizuizini nchini mwao ambapo hivi sasa inajadiliwa iwapo
waachiliwe chini ya sera ya usuluhishi ya taifa.
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
Thomas Lubanga akisikiliza hukumu ya kesi yake mjini The
Hague tarehe 10 Julai 2012.
Thomas Lubanga Dyilo : kiongozi wa zamani wa waasi wa Vikosi
vya Kizalendo vya Ukombozi wa Congo (FPLC) ni mtu pekee hadi sasa aliyepatikana
na hatia katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na hivi sasa yuko kwenye
gereza la Schveningen karibu na The Hague.Alihukumiwa kifungo cha miaka 14
gerezani hapo mwezi wa Machi mwaka 2012 kwa kuwaandikisha askari watoto
mashariki ya Congo.
Germain Katanga : Akiwa kama kiongozi wa kundi la
Upinzani la Kizalendo la (FRPI) huko Ituri anashtakiwa kwa kuhusika huko Katanga kwa mauaji makubwa ya mashariki ya Congo hapo
mwezi wa Februari mwaka 2003.Kesi yake imeahirishwa hadi mwezi wa Machi.
Mathieu Ngudjolo :
Kiongozi wa kundi la Muungano wa Kitaifa la (FNL) mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokorasi ya Congo ni
mshtakiwa mwenza katika kesi ya Katanga
lakini aliachiliwa huru hapo mwezi wa Disemba mwaka 2012 kutokana na ukosefu wa
ushahidi.
Bosco Ntaganda :
Kiongozi wa kundi la wanamgambo la Ulinzi wa Taifa wa Wananchi (CNDP) yuko
kizuizini tokea mwaka 2013 baada ya kujisalimisha mwenyewe huko The
Hague.Anashtakiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu katika
mzozo wa jimbo la Ituri. Baadae akiwa kama
kamanda wa kundi la waasi la M23 alieneza hofu na vitisho mashariki ya
Congo.Kesi dhidi yake inatarajiwa kuanza kusikilizwa hapo mwezi wa Februari
mwaka 2014.
Sylvestre Maudacumura
: Anayedaiwa kuwa kamanda wa kundi la Vikosi vya Demokrasia vya Ukombozi wa Rwanda (FDLR)
anakabiliwa na makosa manane ya uhalifu wa kivita ukiwemo ubakaji, utesaji na
mauaji.
Rais wa sasa wa Kenya
anatuhumiwa kwa kutowa ushirikiano wake katika uhalifu dhidi ya ubinaadamu
wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008.Mchakato wa kesi
yake umeanza tarehe nne mwezi wa Februari mwaka 2014.
Makamo wa Rais wa
Kenya William Samoei Ruto na mtangazaji wa radio Joshua Arap Sang wanakabiliwa
na mashtaka ya mauaji, kuhamisha watu na ukandamizaji.Mchakato wa kesi hiyo
umekuwa ukisikilizwa tokea mwezi wa Septemba mwaka 2013.Ruto hivi sasa
analazimika kushiriki kwenye kesi hiyo kwa kupitia kiungo cha mawasiliano ya
video kutoka Kenya.
Walter Osapiri
Baraza: Waranti wa kukamatwa kwa mwandishi huyo wa habari umetolewa mwezi wa
Oktoba mwaka 2013.Baraza anatuhumiwa kushirikiana na maafisa wa serikali
kuwayumbisha mashahidi katika kesi dhidi ya Kenyatta na Ruto.Waranti wa
kukamatwa kwa Baraza ni wa kwanza kutolewa kuhusu suala la kuyumbisha
mashahidi.
Saif Al - Isalm na Abdullah Al- Senussi - Mtoto huyo wa
kiume wa aliekuwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi anashtakiwa katika
mahakama ya nchini mwake Libya na haitaki kumfikisha kwenye mahakama ya
kimataifa ya ICC huko The Hague.Anashtakiwa pamoja na mkuu wa usalama wa zamani
al-Sanusi kwa kutowa ushirikiano wao katika mauaji na ukandamizaji wakati wa
mapinduzi nchini Libya.
Hapo mwezi wa Januari mwaka 2013 Mwendesha Mashtaka Mkuu wa
ICC Fatou Bensouda ametangaza uchunguzi wa uhalifu wa kivita nchini Mali ambao umefanyika kati ya waasi wa itikadi
kali za Kiislamu na jeshi la serikali ya Mali kaskazini mwa nchi hiyo. Hadi
sasa hakuna kundi linalowajibishwa mbele ya mahakama hiyo ya ICC.
Omar Hassan al Bashir anamfuatia Kenyatta kuwa kiongozi wa
pili madarakani kushtakiwa na mahakama ya ICC.Hata hivyo tafauti na washtakiwa
wa Kenya anagoma kutowa
ushirikiano wake kwa mahakama hiyo ya The
Hague .
Nchi nyengine pia
zinaapuuza waranti wa kumkamata na zinamruhusu Bashir kuingia nchini humo bila
ya bughudha.
Kesi dhidi ya waziri
Ahmad Muhammad Harun na Abel Raheem Muhammad Hussein na ile nyengine dhidi ya
anayedaiwa kuwa mkuu wa kundi la wanamgambo wa Janjaweed Ali Kushayb haikuweza
kusikilizwa kwa sababu ya kushindwa kufikishwa washtakiwa mahakamani.
Vingozi wengine
wawili wa waasi kutoka Dafur wanaoshtakiwa Abdallah Banda na Saleh Jerbo tayari
wamekufa.
Joseph Kony,Vincent Otti, Okot Odhiambo na Dominic Ongwen :
Waranti wa kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la waasi la LRA na makamanda wake
wengine watatu tayari ulikuwa umetolewa na mahakama ya ICC tokea mwaka
2005.Hivi karibuni serikali ya Marekani ilitangaza kwamba inausaidia Umoja wa
Afrika kwa wanajeshi 120 katika msako wa waasi hao.Kundi la LRA pia limekuwa
likiendesha harakati zake kwa muda mrefu mashariki ya Congo,Sudan na Jamhuri ya
Afrika ya Kati.
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jean- Piere Bemba : Kesi ya Makamo wa Rais wa zamani wa
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ilianza hapo mwaka 2010.Bemba anatakiwa ajibu
mashtaka ya matumizi ya nguvu yaliofanywa na jeshi lake la waasi huko Jamhuri
ya Afrika ya Kati hapo mwaka 2002 na mwaka 2003.Akiwa kama mkuu wa kundi la
Vuguvugu la Ukombozi wa Congo (MLC) Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alimuomba
asaidie kuzima mapinduzi ya kijeshi nchini humo.Mwishoni mwa mwaka 2013
aliongezewa mashtaka ambapo yeye na wakili wake Aime Kilolo pamoja na wasaidizi
wake wengine watatu inasemekana wametowa ushahidi wa uongo na kushawishi
mashahidi.
Kwa msaada wa VOA






0 comments:
Post a Comment