Na Kibindo,Zanialy
HABALI kupitia mitadao ya kijamii zimekuwa mkombozi na vyanzo
muhimu vya habari kutokana na ufanisi na uwezo wake wa kufikisha habari toka
sehemu mbalimbali za Tanzania na nje ya Tanzania kwa haraka na muda muafaka
uwezo ambao vyombo vya habari kama Radio,Televisheni pamoja na magazeti havina.
Aidha vyombo hivi vimekuwa mkombozi
kutokana na kukosekana kwa sheria ya moja kwa kwa moja ya kuvibana vyanzo hivi
vya habari kama ilivyo kwa sheria za magazeti na vyombo vya utangazaji yaani
Radio na Televisheni.
Hali inayovipa nafasi vyanzo hivi vya
habari kuwa huru katika utoaji wa habari ambazo Radio na Televisheni na
magazeti zisingeweza kutoa kwa kuofia kwenda kinyume na sheria zinazoongoza
vyombo hivyo mfano sharia ya magazeti ya mwaka 1976 inayolalamikiwa kila uchao.
Uhuru huu wa habari za mitandaoni wakati
mwingine umekuwa ukitumika vibaya na baadhi ya watu kwa kuanzisha
mitandao iliyojaa picha za ngono,stori za maisha ya watu ,video za ngono huku mambo
yenye tija kwa jamii kama vile elimu ya kilimo bora,bei za bidhaa
masokoni,ujasiliamari zikinyimwa nafasi.
Dhana ya habari kwamanufaa ya umma
imepuuzwa kinachotazamwa sasa ni kipi kinapendwa zaidi kwa lengo la kupata
matangazo kutokana na kuwa na wafuatiliaji wengi dhana hii haipaswi kuungwa
mkono hata kidogo,Tusikubali mustakabari wa maisha ya watazania yakachezewa na
watu wachache kwa manufaa yao binafsi.
Imekuwa ni kawaida sana kwa blog za
watanzania kujaa story zinazohusu maisha binafsi ya watu,picha za uchi,habari
za chuki,kuchafuana,unafiki ili mradi mtu amejisikia kuweka habari ianayomjia
kichwani mwake bila kujali imani kubwa iliyopewa mitandao hiyo.
Jambo kubwa la kusikitisha mitandao hiyo
yenye habari,picha na video chafu kuwa na wapenzi wengi vijana wakiwa wengi
zaidi,hali hii inasikitisha sana,wapi tunalipeleka taifa hili,nini mustakabali
wa maisha ya vijana wa kitanzania,vizazi vya namna gani tunaviandaa.
Sina lengo la kuunga mkono moja kwa moja
uthibiti wa matumizi ya mitandao kwa kuwa ni kinyume na haki za watanzania
iliyobainishwa kwenye katiba ,lakini kwa hali hii ipo haja ya kutafuta namna
kusimamia maudhui yanayowekwa kwenye mitandao kwa manufaa ya umma.
Licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa
na Tume ya udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA),Ikiwemo uendeshaji wa semina
na warsha mbalimbali kwa wamiliki wa blog lengo likiwa ni kusisitika matumizi
sahihi ya mitandao kwa mustakabali wa taifa.
Aidha kampeni mbalimbali zinafanywa
kusisitiza matumizi mzuri ya mitandao kukifuatiwa na kauli mbiu mbalimbali kama
vile ukiona ujumbe wa chuki,uchochezi na uongo futa delete kabisa ili mradi tu
kuhakikisha uhuru wa habari mitandaoni unatumiwa vyema.
Licha ya jitihada hizo bado matumizi
mabaya ya mitandao yanashamiri hususani uwepo wa picha zisizofaa
mitandaoni,habari za uongo, udaku ukitawala na huku mambo ya msingi kwa
maendeleo ya watu a taifa kwa ujumla kutopewa kipaumbele.
Kwa mantiki hii ipo haja sasa ya
kusajili, kutoa mafunzo ya kimaadili na kitaaluma kwa wamiliki wa Mitandao ya
kijamii nchini ili mitandao hiyo ilete mchago chanya kwa maendeleo ya Taifa
hili na si kuwa chanzo cha kuporomosha
maadili ya vijana wetu,kusababisha chuki na madhara mengineyo.
0764-784649
0 comments:
Post a Comment