TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Polisi nchini linapenda kuutaarifu
umma kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai
(DCI) Robert Manumba amefikia umri wa kustaafu kisheria ambao ni
miaka sitini (60) katika utendani wake wa kazi.
Aidha, katika utumishi wake ndani ya Jeshi la
Polisi amefanya kazi katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Chumba cha kupokea
mashtaka kuanzia mwaka (1976 – 1977), mwendesha mashtaka wilaya ya Kibondo na
Kasulu mkoani Kigoma, (1977 – 1984), Mkufunzi katika chuo cha polisi Dar es
salaam, (1984 – 1987), Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Magomeni na Kinondoni na
Naibu Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es salaam (1987 –
1993),
Pia, amewahi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa
wa Arusha, ( 1993 – 1995), Mkufunzi mkuu wa Chuo Cha Polisi Moshi (
1995 – 1996), Mkuu wa kitengo cha Fraud makao makuu ya upelelezi, (1996 –
1997), Mkuu wa kitengo cha usalama wa nchi, intelijensia na madawa ya kulevya
makao makuu ya upelelezi (1997 – 2001) na kuwa msaidizi wa
mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini (2001 – 2006). Kuanzia mwaka
2006 hadi anastaafu, alikua Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini.
Aidha, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP)
Said Mwema, amemshukuru na kumpongeza Manumba anayestaafu kwa kulitumikia
taifa katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi kwa weledi na
uwaminifu mkubwa wakati wote alipokuwa mtumishi ndani ya Jeshi la Polisi.
Pia, amemtaka kuendelea kuwa msaada kwa Jeshi
la Polisi kwa kutoa ushirikiano wa namna yoyote ile unaoweza kusaidia kupunguza
uhalifu hapa nchini kwasababu suala la usalama ni taaluma kama
zilivyo taaluma zingine, na taaluma hiyo wanayo watu wachache.
Hata hivyo, wakati tataratibu wa uteuzi wa
mkurugenzi wa upulelezi ukiendelea, mkuu wa ufuatiliaji na tathimini
CID makao makuu, kamishina Isaya Mungulu, atakua akikaimu nafasi
hiyo.
0 comments:
Post a Comment