Mahakama
Kuu ya Tanzania imemzuia Jaji Francis Mutungi na Ofisi ya Msajili wa
Vyama vya siasa nchini au Wakala wake yeyote yule kutoa fedha za ruzuku
za Chama cha Wananchi (CUF), na kumpa Prof. Ibrahim Lipumba mpaka hapo
mashauri ya msingi yanayoendelea Mahakamani yatakaposikilizwa.
Zuio
hilo limetangazwa leo Mei 29, 2018 na Jaji Wilfred Dyansobera katika
Mahakama hiyo na kusisitiza kwamba, maombi ya CUF ya kulinda fedha hizo
yana nguvu za kisheria.
Taarifa
za chama zinaeleza kuwa hadi amri hiyo ya Mahakama inatolewa, Jaji
Mutungi na Ofisi yake ya Msajili wa Vyama imeshamruhusu Prof. Lipumba
kuchukua zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 na fedha hizo zimekuwa zikiwekwa
kwenye akaunti zisizotambuliwa na Bodi Halali ya Udhamini ya chama na
kisha kuhamishiwa kwenye akaunti za watu binafsi akiwemo Prof. Lipumba
Mwenyewe.
Shauri
kuhusu uhalali wa Bodi ya Wadhamini linaendelea kusikilizwa na
inatarajiwa kuwa shahidi wa tatu wa upande wa Chama ataanza kutoa
ushahidi wake mwezi Juni mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment