![]() |
| USS Indianapolis - picha ya mwaka 1937 |
Manowari ya jeshi la Marekani ya USS
Indianapolis ambayo ilizama wakati wa vita vya pili vya dunia,
imepatikana kwenye bahari ya Pacific, Miaka 72 baada ya kuzamishwa na
nyambizi wa Japan.
USS Indianapolis ilikuwa ikirejea kutoka
oparesheni ya siri ya kupeleka sehemu za kunda bomu la atomic ambalo
baadaye lilitumiwa huko Hiroshima.Manowari hiyo ilipatikana kilomita 5.5 chini ya bahari.
Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft Paul Allen, ambaye aliongoza kikosi cha kutafuta manowari hiyo alisema ugunduzi huo ni wa kutia moyo.
USS Indianapolis iliharibiwa tarehe 30 Julai mwaka 1945 katika habari ya Ufilipino kati ya Guam na Leyte baada ya kugongwa na kombora kutoka kwa nyambizi ya Japan.
Kulikuwa na wanajeshi 1,196 ndani ya manowari hiyo na ni kati ya wanajeshi 800 na 900 walinusurika kuzama.
Lakini manowari hiyo haikutuma ishara na hadi wakati masura walipatikana siku nne baadaye ni watu 316 tu waliopatikana wakiwa hai katika eneo hilo lenye papa wengi.
Meli hiyo ni maarufu kwa kufanya safari ya siri ya kusafiirjha sehemu za kuunda bomu la atomic lilifahamika kama "Little Boy" .
Bidhaa hizo zilipelekwa katika kisiwa cha Tinian
kwenye kambi ya jeshi la Marekani ambayo ilifanya shambulizi la kwanza
na bomu la nyuklia.
Siku nne baadaye Indianapolis ilizama chini ya wiki moja kabla ya bomu hilo la nyuklia ililosaidia kuunda kuharibu mji wa Hiroshima.
Siku nne baadaye Indianapolis ilizama chini ya wiki moja kabla ya bomu hilo la nyuklia ililosaidia kuunda kuharibu mji wa Hiroshima.
TAFADHARI TOA MAONI YAKO HAPA

0 comments:
Post a Comment