Akiongea na Waandishi wa Habari Dar es salaam, Naibu Waziri Dk. Hamisi Kigwangallaamesema ‘Takwimu za wiki iliyopita zinaonyesha kuwa kuanzia tarehe 22 hadi 28 ya mwezi Februari 2016, idadi ya wagonjwa wapya walioripotiwa ni 473, na kati yao watu 9 walipoteza maisha.
Jumla ya Mikoa 12 nchini iliripoti wagonjwa katika kipindi cha juma moja lililopita ambapo Mkoa wa Mara uliripoti idadi kubwa zaidi ya wagonjwa ambao ni 125, Iringa 64, Mwanza 59, Morogoro 44, Mbeya 29, Dar es salaam 25, Arusha 18, Kigoma 8, Rukwa 6, Simiyu 6 na Singida 2
Wizara inaendelea kutoa rai kwa jamii, Wataalamu na viongozi katika ngazi zote kwamba kila mmoja wetu atimize wajibu wake katika harakati za kuudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu


TAFADHARI TOA MAONI YAKO HAPA
 
Top