Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) juzi  ilitaja majina ya kampuni 43 na wamiliki wa makontena 329 ambayo yalipitishwa bandarini bila kulipiwa ushuru, na kufichuliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk. Philip Mpango alisema Mamlaka hiyo iliagizwa na Waziri Mkuu Majaliwa kuchukua hatua mara moja kwa kufuatilia na kubaini wamiliki wa Bandari Kavu (ICD) zilizohusika katika kashfa hiyo.

Alisema mbali na hilo walitakiwa kuwatambua wamiliki wa makontena hayo, bidhaa zilizokuwemo, kuwalipisha wahusika kodi iliyokwepwa pamoja na kuwachukulia hatua watumishi waliohusika na upotevu huo.

Dk. Mpango aliyataja majina ya makampuni na watu binafsi na idadi ya makontena waliyopitisha bila kulipia ushuru (katika mabado) kuwa ni:-
  1. Lotai Steel Tanzania Ltd (100)
  2. Tuff Tryes Centre Company Ltd (58)
  3. Binslum Tyres Company Ltd (33)
  4. Tifo Global Mart Tanzania Company Limited (30)
  5. IPS Roofing Company Limited (20)
  6. Rushywheel Tyre Centre Co Ltd (12)
  7. Kiungani Trading Co Ltd (10)
  8. Homing International Limited (9)
  9. Red East Building Materials Company Ltd (7)
  10. Tybat Trading Co Limited (5)
  11. Zing Ent Ltd (4)
  12. Juma Kassem Abdul (3)
  13. Salum Link Tyres (3)
  14. Ally Masoud Dama (2)
  15. CLA Tokyo Limited (2)
  16. Farid Abdullah Salem (2)
  17. Salum Continental Co Ltd (2)
  18. Zuleha Abbas Ali (2)
  19. Issa Ali Salim (2)
  20. Snow Leopard Building (2) 
  21. Abdulaziz Mohamed Ally
  22. Ahmed Saleh Tawred 
  23. Ali Amer 
  24. Ally Alhamdany 
  25. Awadhi Salim Saleh 
  26. Faheed Abdallah Said 
  27. Hani Said 
  28. Hassan Hussein Suleyman 
  29. Hamud Suleiman Enterprise 
  30. Kamil Hussein Ali 
  31. Libas Fashion 
  32. Nassir Salehe Mazrui 
  33. Ngiloi Ulomi Enterprises Co Ltd 
  34. Omar Hussein Badaway 
  35. Said Ahmad Hamdan 
  36. Said Ahmed Said 
  37. Salumu Peculiar Tyres 
  38. Sapato N. Kyando 
  39. Simbo Yonah Kimaro 
  40. Strauss International Co. Ltd 
  41. Swaleh Mohamed Swaleh
Alisema kwa ujumla, makampuni hayo yalipitisha makontena 329 ambayo yaliondolewa kinyume cha taratibu kutoka ICD ya Azam inayomilikiwa na Said Salim Bakhresa And Company Limited.

Dk. Mpango alisema bidhaa zilizokuwemo ndani ya makontena hayo ni pamoja na matairi ya magari, samani mbalimbali, betri za magari, vifaa vya ujenzi, nguo na bidhaa zingine mchanganyiko.

0 comments:

 
Top