Marekani Yataka Wananchi Wake Kuondoka Burundi
Serikali ya Marekani imewataka wananchi wake kuondoka nchini Burundi kufuatia mashambuliano makali baina ya wanamgambo na polisi.Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema imetoa amri ya kuondoka maafisa wake ambao si wadharura na wanafamilia wakati ghasia za kisiasa zikiendelea nchini humo.
Ghasia na mauaji yamekuwa yakiendelea nchini Burundi kufuatia uchaguzi uliopingwa na jaribio la mampinduzi la mwezi Mei mwaka huu.
Ubalozi wa Marekani unaweza kutoa huduma chache za dharura kwa raia wa Marekani nchini Burundi kama ilivyoelezwa katika onyo la usafiri lililotolewa na wizara ya mambo ya nje.
Siku ya Ijumaa zaidi ya watu 80 waliuwawa wakati watu wenye silaha walipovamia eneo la jeshi katika mji mkuu wa Bujumbura
DW.
0 comments:
Post a Comment