Klabu ya soka ya Arsenal yakaa kileleni mwa ligi ya England baada ya kuichapa timu inayoburuza mkia ya Aston Villa bao 2-0 huko Villa Park .
Washika bunduki hao wa London walipata mabao yao kupitia kwa Olivier Giroud kwa mkwaju Penati na Aaron Ramsey kupiga la pili katika dakika ya 38 ya mchezo
Kwa upande wao Majogoo wa Anfield, Liverpool walinusurika kichapo kutoka kwa West Bromwich Albion baada ya Mchezaji alietoka Benchi Divock Origi kusawazisha bao katika dakika za mwisho na kuufanya mchezo kumalizika kwa sare ya 2-2.
Huko White Hart Lane, lile wimbi la Tottenham la kutofungwa katika Mechi 14 za Ligi lilimalizwa Jana baada ya Newcastle kuwachapa 2-1.
Newcastle walitoka nyuma kwa Bao la Dakika ya 39 la Erik Dier na kufunga katika Dakika ya 74 kupitia Aleksandar Mitrovic na Ayoze Perez, Dakika ya 93, Wawili hao wote wakitokea Benchi, na kushinda 2-1 na kujikwamua kutoka Timu 3 za mkiani.
0 comments:
Post a Comment