Image copyright
Rais wa Chama cha Soka Ujerumani DFB- Wolfgang Niersbach amejiuzulu kwa tuhuma za ukwepaji kodi na kujihusisha na rushwa.

Wolfgang Niersbach
Inadaiwa kulitumika rushwa kwa maafisa wa shirikisho la soka duniani katika mchakato wa kuipa Ujerumani zabuni ya kuwa wenyeji wa kombe la dunia 2006.
Tarehe 3 Novemba polisi wa Frankfurt walivamia makao makuu ya chama cha soka Ujerumani kwa uchunguzi wa madai ya ukwepaji kodi kunakokihusu chama hicho kuhusiana maandilizi ya kombe la dunia.
Chama cha soka cha Ujerumani (DFB) kilikana madai hayo mwezi uliopita na Wolfgang Niersbach amesema "Mimi nilihusika katika jitihada kwa ajili ya Kombe la Dunia 2006 kuanzia siku ya kwanza mpaka nyaraka za mwisho za majira zilizowezekana ziliwasilishwa,"
Niersbach alisema."Napenda kuweka wazi bila makosa kwa mara nyingine tena kulikua hakuna maarifa ya nyuma kwa kuwa mtiririko wa malipo uliku unaonekana."
Pia kiongozi huyu akasisitiza kwa kusema yeye alichukua wajibu wa kisiasa kwa malipo kwa Fifa yenye thamani ya Euro 6.7m (£ 4.9M) Nyumba za Niersbach, mtangulizi wake Theo Zwanziger, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Horst Schmid, zilifanyiwa uchunguzi.
 Katika taarifa ya Ofisi mwendesha mashitaka alisema kufunguliwa uchunguzi katika madai ya ukwepaji kodi kubwa wanaohusishwa na Kombe la Dunia nchini Ujerumani mwaka 2006.

0 comments:

 
Top