Wataalamu wa jiolojia wameitwa kuchunguzwa ni jinsi gani ardhi ilipasuka na kumeza magari 12 katika maegesho ya magari jijini Mississippi.
Shimo kubwa, la urefu wa futi 400 (120m) na upana wa futi 35 (11m), lilitokea baadaye Jumamosi katika eneo la Meridian, karibu na barabara kuu ya Alabama.
Eneo hilo limekuwa likipokea mvua kubwa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kwa mujbiu wa gazeti la Meridian Star.
Hakuna aliyejeruhiwa katika kisa hicho, na wahandisi wanatarajiwa kudadisi uthabiti wa ardhi eneo hilo leo.
Bw Buck Roberts, tmkurugenzi wa usalama wa umma eneo la Meridian, aliambia gazeti hilo kwamba hilo halionekani kuwa shimo la kawaida ambalo hutokana na sehemu inayohifadhi maji chini ya ardhi kukauka na ardhi kuporomoka.
0 comments:
Post a Comment