"Tutapunguza misamaha ya kodi kufikia asilimia moja (1%) tu ya pato la taifa (au chini ya hapo) kama inavyoshauriwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Wenzetu Kenya na Uganda wameweza. Tanzania inapoteza zaidi ya Shilingi trilioni moja nukta nne kila Mwaka kutokana na misamaha holela ya kodi. - Tukilitekeleza hili pekee, tutaweza kulipa Deni la Walimu la Shillingi Bilioni Thelathini na Tatu na bado chenji kubwa ikabaki kuboresha maslahi ya Polisi, Madaktari, n.k. - Kwa mujibu wa Wizara ya Fedha, kiasi cha misamaha ya kodi katika mwaka wa fedha 2014/15 kilikuwa Shilingi Trilioni 1.419. Katika kipindi hicho, serikali ilitegemea kukusanya takriban Shilingi Trilioni 10 kama kodi. Hii inaonyesha kwamba kiasi cha misamaha kilikuwa asilimia 14 ya mapato ya kodi.
Kuhakikisha kwamba misamaha yote ya kodi inawekwa wazi na inakaguliwa na mamlaka ya kodi (TRA), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha Za Serikali (CAG), pamoja na Kamati husika za Bunge".
0 comments:
Post a Comment