Mhe. Edward Ngoyai Lowassa akiwasili katika viwanja vya Shule ya msingi Tunduma,Jumamosi 17/10/2015, lakini mkutano uliahirishwa mpaka kesho saa 3 asubuhi kutokana na vipasa sauti kupata hitilafu na kugoma kutoa sauti,hata hivyo mafundi walifanya jitihada mbalimbali lakini hazikuzaa matunda,ndipo mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe. Freeman Mbowe akaahirisha mkutano huo,hadi kesho Jumapili 18/10/2015 


















MGOMBEA wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema ambaye anaungwa mkono chini ya Mwavuli wa UKAWA Edward Lowassa ni kama amehindikana ndivyo naweza kusema baada kuismiamisha maeneo ya Tunduma mkoani mbeya.
           Taarifa kutoka Tundunduma zinasema tangu asubuhi mji mizma wa Tunduma zilikuwa zimama huku barabara zikifungwa huku vijana wakiwa barabarani wakishangilia nyimbo wakisema “Rais Rais Rais wetu kaja,Rais wetu kaja”
Huku Jeshi la Polisi Mkoni mbeya alikiwa limezidiwa nguvu na Umati mkubwa wa watu, waliokuwa barabarani wakifunga barabara,
          Lowassa ambaye anaungwa mkono na vyama vya NCCR-Mageuzi,Chama cha Wananch CUF pamoja na NLD aliwataka wakazi wa Tunduma kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 25 Octoba na kumchagua kwa wingi ili aingia madarakani apambane na Tatizo kubwa la Umasikini ambalo limekuwa kama laana kwa watanzania,
         Amesema anafahamu jinsi watanzania walivyokata Tamaa ya Maisha kutokana na Umasikini ndio maana nafsi imemtuma.

0 comments:

 
Top