KILA OCTOBA 08 NI SIKU YA MACHO DUNIANI, FAHAMU HAPA NAMNA YA KULINDA AFYA YA MACHO YAKO LEO
Octoba 08 ya kila mwaka duniani kote huadhimisha siku ya macho duniani, siku ambayo huadhimishwa kwa lengo la kuongeza uelewa kwa umma duniani kote kuhusu kuzuia matatizo ya macho pamoja na matibabu yake pia.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kuwa kila sekunde tano mtu mmoja duniani anakuwa kipofu.
Aidha kwa mujibu wa WHO wanasema kuwa kila dakika moja duniani kote mtoto mmoja anakuwa kipofu.
Pamoja na hayo, WHO inakadiria kwamba zaidi ya watu milioni saba hupata matatizo ya macho na kuwa vipofu kila mwaka, huku ikielezwa kuwa asilima 80% ya kesi za upofu huweza kuepukika.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo huweza kukuepusha na kukumbwa na matatizo ya macho:-
Kwanza kabisa ili kuepuka matatizo ya macho ni muhimu sana kujenga utaratibu wa kufanya uchunguzi wa macho yako mara kwa mara ili kutambua kama utakuwa na magonjwa yanayoweza kusababisha upofu.
Epuka kufanya kazi zako sehemu ambayo itakuwa na mwanga hafifu hii itasababisha macho yako kutumia nguvu nyingi sana katika kuona.
Acha kuangalia moja kwa moja mwanga mkali kama jua au moto wa kuchomelea na kama utakuwa unafanya kazi kwenye kifaa kinachotoa mwanga ni vyema kukaa umbali wa sentimita 25 mpaka 30.
Zuia macho yako kwa miwani ya jua ukiwa unaendesha pikipiki, baiskeli hii itasaidia macho kutopigwa na vumbi au kuingiwa na wadudu machoni.
Kuna baadhi ya watu hupenda kusoma vitu, huku wakiwa wanatembea, hii tabia nayo si nzuri kwa afya ya macho.
Epuka kutumia taulo za kuogea kwa kushare, kwani ugonjwa wa macho unaweza kuhama kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia hiyo.
Leo siku ya macho duniani nimeona nishare na wewe haya machache kuhusu namna ya kulinda macho yako,
Source ni Dk MANDAI
0 comments:
Post a Comment